TANESCO YATOA NAMBA ZA SIMU KWA AJILI YA HUDUMA ZA DHARURA MIKOANI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linautaarifu umma kuhusu uwepo wa hitilafu katika kituo chetu cha miito ya simu (call center) na hivyo kupelekea kutopatikana kwa namba yetu ya huduma kwa wateja 0748550000.
Tunawashauri wateja wetu kutumia namba za huduma kwa wateja za mikoa husika kwa ajili ya kutoa taarifa za changamoto mbalimbali kama orodha inavyoonesha hapa chini, vilevile kupitia namba ya WhatsApp 0748550000, Nikonekt App au Makundi ya huduma kwa wateja ya WhatsApp ya maeneo husika.
Wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kurekebisha hitilafu hiyo na pindi itakapokamilika tutawataarifu.
Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.
No comments