MKOA WA DAR ES SALAAM WAJIPANGA MAPOKEZI WAKUU WA NCHI MKUTANO WA NISHATI
ABRAHAM NTAMBARA NA TUNU BASHEMELA
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema
maandalizi ya mapokezi ya Wakuu wa Nchi za Afrika kuelekeza Mkutano wa viongozi
hao kuhusu Nishati utakao ongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yamefikia zaidi
ya asilimia 70.
RC Chalamila alibainisha hayo jana akizungumza na
waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ukaguzi wa maeneo
mbalimbali ambayo watapita wageni wa Mkutano huo wakiwemo Marais wa Afrika
zaidi ya 10.
Maeneo aliyotembelea na kufanya ukaguzi ni Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Barabara ya Nyerere kutoka JNIA
hadi Posta, Viwanja vya Karimjee Pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Juluius Nyerere (JNICC) ambapo mkutano huo utafanyika kuanzia Januari 27 hadi
28 mwaka huu.
Alisema kuwa Serikali inaratibu mkutano huo Mkubwa wa
Nishati barani Afrika, hivyo kuelekea mkutano huo kama Mkowa wamepewa majukumu
ya kufanya ambapo alieleza kuwa moja ya majukumu hayo ni kuhakikisha usafi wa
maeneo yote nyeti ambayo wageni watapita.
“Serikali inaratibu Mkutano Mkubwa wa Nishati barani
Afrika, Mkutano huu ni wakuharakisha upatikanaji wa Nishati kwa watu milioni
300 barani Afrika. Hivyo katika maandalizi haya Mkoa umepewa majukumu ya
kufanya ikiwemo kufanya usafi,” alisema RC Chalamila.
RC Chalamila alieleza kuwa Mkoa umejipanga kuhakikisha
meneo yote nyeti yanakuwa safi ambapo alitaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni
Pamoja na Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA), Barabara ya Nyerere hadi
Posta, Coco Beach na Karimjee.
Hivyo alisema vyombo vya dola kwa kushirikiana na
wananchi Jumamosi mwishoni mwa wiki hii watafanya usafi mkoani humo na kuwataka
wananchi kutoshangaa wala kuogopa watakapo viona vyombo hivyo vikifanya usafi
mitaani.
Kadhalika alisema kuwa uongozi wa Mkoa umepanga
kuhakikisha majengo yote yaliyopo kando kando ya badabara ambapo wageni
watapita yapakwe rangi, hivyo wameagiza wamiliki wote wa majengo hayo kuyapaka
rangi ili yawe na mwonekano mzuri na kuweka taswira nzuri ya Jiji.
Hivyo alitumia fursa hiyo kuwaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha majengo hayo yote yanapakwa rangi.
Kadhalika katika kuutangaza Mkutano huo, RC Chalamila
alisema mabango yanayohusu mkutano yatawekwa katika maeneo mbalimbali yam ji
ambapo alisisitiza kuwa malengo ya mkutano na kufikisha Nishati ya Umeme kwa
watu milioni 300 jambo ambalo linaunga mkono Kampeni ya Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
Akizungumzia kuhusu paking za magari, alisema kuwa
hadi kufikia Januari 20 Maliro yote hayataruhusiwa kupaki pembezoni mwa
barabada hususan katika Barabara ya Nreyeye, hivyo aliwataka wamiliki wa Malori
kuhakikisha wanatafuta sehemu ya kuyapaki.
Kwamba Malori hayo kupaki pambezoni mwa Barabara ni
saw ana uchafu jambo ambalo linachafua taswira ya Jiji ambapo alisisitiza kwa
hadi kufikia Januari 20 mwaka huu Malori hayo hayatakiwi kuonekana pembezoni
mwa Barabara.
Kuhusu ufungaji wa taa, alieleza kuwa zaidi ya taa 300
zitafungwa Barabara ya Nyerere hadi Posta na kwamba hadi kufukia Januari 20
nazo pia zitakuwa zimeshafungwa kwa ajili yakupendezesha taswira ya Mji
sambamba na kuimarisha usalama kwa ajili ya wageni.
Hivi karibuni akieleza sababu za Tanzania kuwa Mwenyeiji wa
Mkutano huu, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano, Waizaya ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Noel Kaganda alisema Tanzania ni
miongoni mwa nchi za Afrika zinazofanya vizuri katika Sekta ya Nishati.
Alisema hadi kufikia Disemba 2024, uzalishaji umeme kwa
Tanzania bara ulikuwa umefikia Megawati 3,169.20, upatikanaji wa umeme
umeongezeka kutoka asilimia 14 mwaka 2011 hadi asilimia 78.4 mwaka 2020. Kwamba
kufuatia Mpango wa Usambazaji Umeme vijijini (REA), takriban vijiji vyote
nchini vimefikiwa
Sababu nyingine ni kuwa Rais Dkt. Samia amekuwa kinara wa
kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo amefanya hivyo kwenye majukwaa mbalimbali ya
kimataifa, ikiwemo COP 27, 28 na 29, Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu
Nishati Safi ya Kupikia (May, Paris), Mkutano wa G20 (Nov, Rio de Janeiro).
Kadhalika Tanzania ina mikakati kabambe ya kuongeza
upatikanaji wa umeme wa uhakika, endelevu na wa gharama nafuu kwa wote hadi
kufikia asilimia 75 ifikapo mwaka 2030 na asilimia 80 hadi ifikapo 2034 kwa
upande wa nishati safi ya kupiki na kushamiri kwa diplomasia, Amani, utulivu,
ukarimu, uzoefu.
No comments