Breaking News

Dkt. Jafo: Bodi Simamieni CAMARTEC izalishe zaidi



Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt.Selemani Jafo ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa  Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kuleta mabadiliko zaidi katika uzalishaji na udhibiti wa zana za kilimo zinazoingia kutoka nje ya nchi ikiwemo kutopata hati chafu sanjari na matumizi sahihi ya fedha. 

Waziri Jafo ameyasema hayo Januari 24, 2025 wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa CAMARTEC, Jijini Arusha ambapo Mwenyekiti wa Bodi hiyo kula kiapo cha Maadili.

Alisisitiza Bodi hiyo kusimamia vema kazi za kituo hicho ikiwemo kuacha  kufanya kazi kwa mazoea  ili kuhakikisha zana za kilimo zinawafikia wananchi wengi hususani wakulima ili waweze kuwa na matumizi sahihi ya zana za kilimo na vema ili kuhakikisha CAMARTEC inapata maendeleo. 

Vilevile Dkt Jafo ameishauri Bodi hiyo kuendelea kutoa ushauri ikiwemo kusimamia Menejinenti na Wajumbe  wake kufanya kazi kwa upendi na nidhamu kazini  ili kuhakikisha wanaleta tija katika kituo hicho ili kuhakikisha wanatoa matunda bora.

"Lazima muwe wabunifu na kujifunza zaidi ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia lazima Bodi hii iendane na wakati katika kusimamia kazi ili CAMARTEC ibadilike katika uzalishaji wa zana za kilimo kwani kilimo ni tija na endapo tukifanya vizuri tutaisaidia Wizara ya Kilimo katika masuala ya ubunifu " Amesema Dkt Jafo.

"Nahitaji mabadiliko katika Bodi hii kwani tangu mwaka 1982 hadi leo hii CAMARTEC imefanya nini katika ubunifu, lakini pia Menejimenti saidieni Bodi kuhakikisha taasisi hii inaenda mbele zaidi ikiwemo matumizi ya usimamizi wa rasilimali haswa katika matumizi ya fedha na kuhakikisha Camartec haipati hati chafu 

Vilevike Dkt Jafo ameziagiza Taasisi zote zilizochini ya Wizara yake  ikiwemo CAMARTEC kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili  ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano ili kiweze kutejeleza majukumu yake ipasavyo katika kuelimisha umma kuhusu jitihada mbalimbali za kuendeleza sekta ya viwanda na biashara. 

Naye Mkurugenzi wa  Sera na Mipango kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Needpeace Wambuya akimwakilisha  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Dkt,Hashil Abdalah amesema  anaamini Bodi hiyo itasimamia kwa ukamilifu tafiti na majaribio ya teknolojia kwa ajili ya zana za kilimo zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchini

Akisoma taarifa ya kituo hicho, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC, Injinia Godfrey Mwinama amesema  Kituo hicho kimefanikiwa kuunda zana mpya 42 zinazozalisha zana mbalimbali kwa ajili ya  kuongeza tija katika kilimo

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya CAMARTEC, Profesa  Valerian Silayo alisema Bodi hiyo imepokea maelekezo yote yaliyitolewa na iko tayari kuyafanyia kazi ili  kuhakikisha CAMARTEC inafikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kusaidiwa upatikanaji wa fedha za kuendesha kituo hicho kwa wakati


No comments