WANANCHI ZAIDI YA 2,300 WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUWAJENGEA SHULE MPYA YA NYAMAGOMA - NGARA
Elimu ni ufunguo wa maisha, Wakati kwako wewe linaweza kuwa jambo la kawaida kuona shule zikiwa karibu yako, kwa wakazi wa Ngara Kata ya Nyamagoma wanafunzi walilazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya KM 40 kila siku kufata elimu ya Sekondari ili waweze kutimiza ndoto zao za maisha ya baadae.
Jitihada mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na viongozi na Mnamo mwaka 2020, Mhe. Ndaisaba Ruhoro ambaye ni mbunge wa Jimbo la Ngara na Diwani wa Kata hiyo Mh Laurent Msongalele walitoa ahadi ya kuwajengea shule ya sekondari iwapo wangechaguliwa kuongoza katika nafasi walizo ziomba na hatimae wakaibuka kidedea ndipo Mbio zikaanza za kutekeleza ahadi zao kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo ambayo yamefanyika Mbunge huyo kijana ameendelea kuwa na kiu ya kuwaletea wanangara maendeleo kupitia Maswali na Michango yake bungeni pamoja na Mbio za Kumkimbilia Mama wa Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae alikubali na kutoa TZS 584,000,000M kufanikisha ujenzi wa shule hiyo.
Ujenzi ulipo kamilika, wananchi walimuomba Mbunge wao kuwasaidia kufanya Sherehe ya Kuwapongeza viongozi wao akiwemo Rais Samia ambae ametoa fedha za kufanikisha ujenzi wa shule hiyo. Mbunge aliridhia ombi hilo na kutoa TZS 5,600,000.00 cash na Mchele kilo 100. Wananchi wamechangia kilo za mchele 650kg, Ng’ombe 4 ambapo wananchi zaidi ya 2,300 walihudhuria na kupata chakula cha kutosha kwa vifijo na nderemo huku wakimwaga pongezi nyingi kwa Rais, Mbunge na Diwani kwa kuwafanyia kazi Nzuri sana.
Ikumbukwe kuwa wanafunzi walilazimika kupita katika eneo lenye milima, Mabonde na ukosefu wa Usafiri, elimu ya Sekondari ilikuwa ni Mateso makubwa kwao na wengi hawakuweza kuhitimu kidato cha nne hivyo kwa furaha hiyo Wananchi hao wameadhimia kuhakikisha wanawachagua viongozi wao hao hao ambao wameweza kutatua kero zao.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/NWdQVSJ
No comments