#KAZIINAONGEA

Idadi kubwa ya vijana nchini imeonesha kuvutiwa na kasi ya utendaji kazi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo Disemba 7,2024 walijitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio za pole zilizopewa jina la Generation Samia Jogging lililofanyika jijini Dodoma.

Vijana hao walionesha mshikamano wa dhati na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia.

Tukio hilo lililovuta hisia za wengi limekuwa nembo ya mshikamano wa kizazi kipya, likidhihirisha jinsi vijana wanavyothamini na kuunga mkono dira ya maendeleo ya serikali.

Wakiwa na ari na nguvu, washiriki walionekana  kuwa na furaha na bashasha, huku wakitoa ujumbe wa kumuunga mkono Rais Dkt. Samia.

Kwa mujibu wa waandaaji, mafanikio makubwa ya tukio hili yanaashiria azma ya vijana kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kushiriki agenda za maendeleo ya taifa na kumuunga mkono  Rais.

Aidha wameahidi kuendeleza matukio zaidi ya aina hii yatakayolenga kuimarisha mshikamano wa kijamii, kukuza ari ya kizalendo, na kuhamasisha jamii kuishi kwa upendo.

*#KAZIINAONGEA*