USHIRIKIANO WA TANZANIA NA KOREA KUSINI, WAZAA MATUNDA.
USHIRIKIANO WA TANZANIA NA KOREA KUSINI, WAZAA MATUNDA.
#KAZIINAONGEA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imenufaika kwa kupata msaada wa Dola za Marekani Milioni 8 kwa ajili ya kujenga Mfumo wa Kusimamia Huduma za Maji katika Mamlaka ya Maji Iringa (Smart Water Management System), kutoka Korea Environmental Industry and Technology Institute (KEITI).
Manufaa haya yametokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Korea na Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo kupitia mfumo huo, Mamlaka ya Maji Iringa (IRUWASA), itakuwa Mamlaka ya Maji ya kwanza nchini kutumia mfumo huo.
Mfumo huo utaongeza ufanisi katika kudhibiti upotevu wa maji, kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuimarisha huduma ya maji nchini ambapo utelezaji wa miradi hiyo utaimarisha huduma za usafi wa mazingira, kuondoa na kutibu maji taka.
Katika kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametembelea na kuongea na Viongozi wa Benki ya EXIM ya Korea ambayo ilitoa fedha za utekelezaji wa miradi ya Majitaka nchini Tanzania yenye jumla ya Dola za Marekani Milioni 248.3.
Mchanganua wa fedha hizo ni kwa Mkoa wa Dar es Salaam Dola za Marekani Milioni 90, Dodoma Dola Milioni 70 na Mkoa wa Iringa Dola Milioni 88.3.
Makamu wa Rais wa Benki hiyo amesema kupitia EDCF na Mifuko mingine Serikali ya Korea itaendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania kupitia Sekta ya Maji katika uwekezaji zaidi wa utekelezaji wa Miradi ya Maji.
Kupitia ziara hiyo ya Aweso nchini Korea Kusini, ameimarisha ushirikiano na Wadau wa maji nchini Korea ambao ni K-Water na Makampuni mbalimbali hali ambayo imefungua fursa zaidi za kushirikiana katika kuwajengea uwezo Watumishi na Taasisi za Maji ikiwa ni pamoja na kuandaa miradi na kutafuta fedha.
*#KAZIINAONGEA*
No comments