TBS YAWAHIMIZA WENYE VIWANDA NA TAASISI KUTHIBITISHA MIFUMO YAO YA UBORA
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limezitaka taasisi, sekta mbalimbali na wenye viwanda kuhakikisha wanathibitisha mifumo yao ya huduma ili kuhakikisha ubora na usalama katika uzalishaji na utoaji huduma.
Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 19, 2024 Jijini Dar es Salaam,Meneja uthibitishaji mifumo ya ubora Bi.Nasra Hussein amesema TBS ina Cheti cha umahiri katika kuthibitisha mifumo, hivyo inapelekea huduma inayotolewa na TBS kuwa na uhakika na kutambulika Duniani kote.
"Faida ya kuthibitisha mifumo ni pamoja na kuaminiwa na wateja wetu kwamba huduma hii inamfumo thabiti na vilevile inasaidia kuweza kupata masoko ndani na nje ya nchi kwasababu huduma tutakazo zitoa pamoja na uzalishaji utakuwa umethibitiwa na mifumo ya ubora". Amesema
Aidha amesema kuna Viwango vya mfumo wa usimamizi wa usalama wa chakula ambao ni hususan kwa wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa bidhaa za chakula.
Amesema kiwango kingine ni usimamizi wa mazingira,kiwango hiki kina umuhimu wa kusimamia usimamizi wa mazingira kwani tumekuwa tukiacha athari katika mazingira kwenye uzalishaji na utoaji huduma zetu.
Amesema kuna kiwango pia cha Usalama mahala pa kazi, hii inahusisha Taasisi, sekta ya wazalishaji na makampuni yote kwani tunafahamu umuhimu wa wafanyakazi na usalama wao katika maeneo ya kazi
"Mfumo huu unahusisha taasisi na viwanda vyote kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wao ili kupunguza ajali na madhara ya kiafya". Amesema
Pamoja na hayo amesema kuna kiwango cha ubora wa elimu katika Taasisi zetu za elimu, huduma hii ni kwa sekta za elimu zote kuanzia shule mpaka vyuo, hii ni muhimu kututambulisha kwamba huduma hii inakuwa inasimamia ubora na kujali masilahi ya wafanyakazi, walimu na wanafunzi wote kwakuzingatia mahitaji maalumu.
Vilevile mifumo mingine ambayo inatakiwa kuthibitishwa ni pamoja na mfumo wa usimamizi wa mazingira, Mfumo wa usimamizi wa nyaraka zetu na mfumo wa ubora wa elimu katika Taasisi zetu za elimu, huduma hii ni kwa sekta za elimu zote kuanzia shule mpaka vyuo,
No comments