Breaking News

RAIS DKT.SAMIA ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 1,548

* Ni katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika

#KAZIINAONGEA

Katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika, mnamo Disemba 9, mwaka 1961, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza msamaha kwa Wafungwa 1,548 ambapo Wafungwa 22 kati yao wameachiliwa huru leo Disemba 09, 2024.

Katika msamaha huo wa wafungwa hao, Wafungwa 1526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.

Taarifa iliyotolewa leo na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inasema, msamaha huo wa Rais Samia ni sehemu ya maadhimisho ya  Miaka 63 ya Uhuru wa anganyika (Tanzania Bara).

“Ni matarajio ya Serikali kuwa, Wafungwa walioachiliwa huru  watarejea tena katika Jamii kushirikiana na Wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani” amesisitiza Rais Dkt. Samia.


#KAZIINAONGEA

No comments