Breaking News

MIAKA 63 YA UHURU WA TANGANYIKA NA MRADI WA UMEME MTO RUFIJI (JNHPP)

 

#KAZIINAONGEA

Huku tukisherehekea Maadhimisho  ya miaka 63 tangu Tanganyika ilipopata Uhuru wake Disemba 9,1964, tunashuhudia mafanikio makubwa katika Uongozi wa Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tangu alipoingia madarakani.

Miongoni mwa mafanikio hayo ni katika miundombinu ya Nishati ya Umeme ya Mradi wa kuzalisha umeme wa Mwalimu Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP), uliojengwa kwenye mto Rufiji.

Mradi huu ni muhimu sana kwa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na Kitaifa wenye uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 2,115,  ikiwakilisha zaidi ya asilimia 60 ya mahitaji ya umeme wa Tanzania ambapo uzalishaji wa umeme huo utakaoongeza uzalishaji wa umeme wa Taifa zaidi ya mara mbili ya ulivyokuwa Unazalishwa hapo awali.

Mradi huu unazalisha umeme wa kutumia maji, ambao ni rafiki kwa mazingira, na unachangia juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kupunguza utegemezi wa vyanzo vya Nishati vinavyotoa hewa ya ukaa, kama makaa ya mawe na mafuta na uleta unafuu ya gharama za umeme.

Mradi wa JNHPP utatoa Nishati ya uhakika na utakuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji wa viwanda, kilimo cha umwagiliaji, na biashara nyingine zinazohitaji umeme wa uhakika na itawezesha upanuzi wa gridi ya Taifa kufikia maeneo ya vijijini.

Mradi huu ni sehemu ya juhudi za Rais Dkt. Samia katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na Nishati ya uhakika kwa umeme, kwa maendeleo ya Viwanda na itapanua wigo na kutoa fursa kwa Wawekezaji kuwekeza nchini.

Umeme huu utatoa unafuu mkubwa wa gharama kwa watumiaji kutokana na kuwa, uzalishaji wake ni wa gharama nafuu ukilinganisha na vyanzo vingine ambapo uniti moja ya umeme unaozalishwa kwa kutumia maji inagharimu Shilingi 36 hadi Shilingi 50, huku umeme unaotumia vyanzo vya mafuta uniti moja inazalishwa kwa gharama ya shilingi 440 hadi shilingi 600.

Gharama za umeme kwa uniti kutokana na vyanzo vingine vya kuzalisha umeme ni upepo ambao gharama zake ni Shilingi 103.5, jua Shilingi 103.5, Makaa ya Mawe Shilingi 114, Jotoardhi Shilingi 118, Nuklia Shilingi 65 na Gesi Shilingi 147.


#KAZIINAONGEA

No comments