Miaka 63 ya Uhuru, Rais Samia aimarisha huduma za afya
Kauli mbiu miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika Disemba 09,2024: "Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo".
***
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha kwa kiasi kikubwa huduma za afya Shinyanga Mjini kwa kukamilisha ujenzi wa Zahanati na vituo vya Afya ambavyo ujenzi wake ulisimama kabla ya kuingia kwake madarakani.
Vituo vya Afya na Zahanati mpya zaidi ya tatu zimejengwa na kukamilika na sasa kuna uhakika mkubwa wa kupata huduma bora za afya.
Katika eneo la Shinyanga Mjini ambalo pia ni jimbo linaloongozwa na Mbunge Patrobas Katambi kumepatikana mafanikio makubwa katika sekta ya afya.
Mafanikio hayo yametokana na Mpango mkakati wa Utekelezaji wa Dira ya maendeleo ya Taifa(2025),Sera ya Afya ya Mwaka(2007),Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka (2020-2025) na Mpango mkakati wa Tano wa sekta ya Afya 2021/22-2025/2026.
Katika kipindi cha uongozi wake, Rais Dkt. Samia ameendelea kutoa fedha za miradi iliyokuwa imekwama, ambapo amefanikiwa kujenga vituo vya Afya hapa kwa thamani ya shilingi milioni 500, kituo cha Afya Lubaga(104,000,000), miradi hii imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi.
Sambamba na hilo ipo miradi minginne ambayo ilikwama kwa muda mrefu ambayo ni Zahanati ya Bushola iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 56, Zahanati ya Masekelo Tshs(70,000,000), Zahanati ya Songambele (Kitangili) Tshs(60,000,000) na Zahanati ya Seseko Tshs(85,000,000).
Vilevile katika kituo cha Afya kambarage amefanikiwa kukarabati wodi na jengo la OPD kwa Tshs (500,000,000). Kufikia 2024/2025 zahanati ambazo zipo kwenye ukamilishaji ni pamoja na zahanati ya Mwamagunguli (kolandoto), Zahanati ya Mwagala (Ibadakuli) na Zahanati ya Ibinzamata (Ibinzamata)
Katika kurahisisha Utoaji wa huduma kwa Wananchi ndani ya Miaka minne(4) Pia amefanikiwa kutoa gari sita za wagonjwa kwenye maeneo tofauti yanayotoa huduma za afya Shinyanga.
Aidha serikali ya Rais Dkt. Samia imefanikiwa kufanya ukarabati katika Hospitali ya manispaa ya Shinyanga kwa kutumia zaidi ya shilingi 1.3billioni.
#KAZIINAONGEA
No comments