DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 KUZINDULIWA NA RAIS DKT.SAMIA 2025.
#KAZIINAONGEA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua rasmi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kati ya Mwezi Mei/Juni 2025 mara baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuijadili na kuidhinisha Rasimu ya Dira ya Maendeleo 2050.
Mpango huu wa kuwepo kwa Dira ya Maendeleo ya Taifa, ni miongoni mwa mikakati ya Rais Dkt. Samia, katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, ambapo amekuwa na maono ya kuona mbali katika utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo ya Taifa.
Maandalizi ya Dira 2050 yanaenda sambamba na maandalizi ya mpango elekezi wa muda mrefu wa maendeleo utakaotafsiri maono na matamanio yaliyopo kwenye Dira 2050.
Akiongea kuhusu tathmini ya mchakato wa uandaaji wa Dira 2050, Jijini Dar es Salaam Disemba 06,2024, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof.Kitila Mkumbo amesema, matamanio na matarajio ya Watanzania wengi kwa miaka 25 ijayo, ni kuona uchumi imara, unaostawi na unaoboresha maisha yao.
Ameongeza kusema kuwa, pia wananchi wanataka kupata huduma bora, utoaji haki pamoja na uthabiti kwenye ulinzi na usalama, sambamba na kuimarishwa kwa maendeleo ya teknolojia na ubunifu, ulinzi na matumizi endelevu ya rasilimali za Taifa.
Waziri Mkumbo amesema kuwa, Wananchi wengi pia wametaja Sekta tano muhimu wanazotaka zitiliwe mkazo kwa miaka 25 ijayo ambazo ni pamoja na kilimo, uzalishaji viwandani, miundombinu, huduma bora za kijamii, madini, mafuta pamoja na gesi, ambapo amewataka Wananchi kushiriki kikamilifu kwenye uzinduzi huo wa Dira ya Maendeleo ya Taifa letu 2050 utakaozinduliwa kati ya mwezi Mei na Juni, 2025.
*#KAZIINAONGEA*
DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 KUZINDULIWA NA RAIS DKT.SAMIA 2025.
Reviewed by Tanzania Yetu
on
December 09, 2024
Rating: 5
No comments