AJALI YA BASI YAUA WATU 11 , KUJERUHI KAGERA
Watu 11 wamefariki dunia huku 16 wakijeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea katika Kijiji cha Kabukome Kata ya Nyarubungo kwenye mlima wa kuanzia pori la Kasindaga lililopo Wilaya ya Biharamulo na Muleba Mkoani Kagera.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amelitaja gari hilo kuwa lina namba za usajili T 857 DHW linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Bukoba ambapo liliacha njia na kupinduka na hatimaye kusababisha vifo vya Watu 11 kati ya hao Wanaume ni wanne Watu wazima na Wanawake watano, Mtoto wa kiume mmoja na Mtoto wa kike mmoja na miili yote ipo Hospitali teule ya Wilaya ya Biharamulo huku kati ya 16 waliojeruhiwa baadhi yao wanaendelea vizuri na muda wowote wataruhusiwa.
Amesema kuwa chanzo cha ajali ni kufeli kwa mfumo wa gari zima "Gari hili lilipotoka Biharamulo kwenda Bukoba lilimpitiliza kituo cha kushuka Mtoto mmoja sasa Ndugu zake wakapiga simu kuwa wamempitisha, Dereva akakutana na Coaster kwenye mlima ule kwa sababu ya haraka akasimamisha gari mlimani konda akashuka na mtoto ili amuwaishe kwenye gari ambalo linawahi Biharamulo kwa bahati mbaya mfumo wa gari ukagoma, mfumo wa breki mfumo wa gia vyote vikagoma gari likaanza kuserereka na likawa limemshinda Dereva likatoka nje ya barabara na kubinuka na Watu wengi wamepoteza maisha kwasababu walilaliwa na gari"
CHANZO - MATUKIO DAIMA
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/sa5H29E
No comments