Waziri Mkuu Majaliwa apongeza mchango wa Sekta ya Madini nchini
Na Mwandishi Wetu Dar es salaam
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameipongeza Wizara ya Madini kwa juhudi mbalimbali inazofanya za kuiendeleza Sekta ya Madini kufikia asilimia 9.0 katika kuchangia kwenye Pato la Taifa huku sekta ikikua kwa asilimia 11.3.
Ameyasema hayo, leo Novemba 19, 2023 wakati wa akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2024 unaendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa, uwepo wa Sera nzuri zenye ushawishi , mazingira salama yenye utulivu na amani, uwepo wa masoko ya uhakika yaliyounganishwa na jiografia nzuri vyote hivyo kwa pamoja vimekuwa vichocheo vikubwa katika ukuaji wa Sekta ya Madini nchini.
Waziri Mkuu Majaliwa amefafanua kuwa , Serikali itaendelea kuboresha miundombinu yote inayohusiana na mnyororo mzima wa thamani madini ikiwa barabara , nishati ya umeme pamoja kuongeza idadi ya vituo vya mauzo na masoko ili kuiweka sekta katika hali ya ubora na ushindani.
Awali, akimkaribisha Waziri Mkuu , Waziri wa Madini , Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kunufaika na rasilimali madini, Wizara imeendelea kuimarisha usimamizi wa shughuli za madini na kuhakikisha wananchi wananufaika naSerikali inapata mapato stahiki.
No comments