#KAZIINAONGEA
 
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Urusi zimejadili kuhusu miradi ya pamoja ya Nishati, Kilimo, Miundombinu na Utalii, hii ni kupitia Mkutano kati ya ofisi ya Waziri Mkuu Tanzania na Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Urusi Maxim Reshetnikov, katika majadiliano yaliyofanyika Oktoba 30,2024  jijini Dar es Salaam.
 
Ujumbe wa Urusi ukiongozwa na Reshetnikov uliwasili nchini Oktoba 28  ili kushiriki katika mkutano wa kwanza wa Tume ya Biashara na Ushirikiano wa Kiuchumi ya Urusi na Tanzania.
 
“Serikali ya Tanzania chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuboresha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na mataifa rafiki, ikiwemo Urusi. 
 
Baada ya mazungumzo hayo  Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Urusi Maxim Reshetnikov Reshetnikov ameeleza kuwa nchi hizo mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji.
 
Kama sehemu ya hili, wamefanya mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kiserikali ya Biashara na Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Urusi na Tanzania ili kuimarisha uhusiano.

"Tuko tayari kusaidia uchumi wa Tanzania kudumisha kasi ya juu ambayo imefikiwa katika sekta ya nishati, kilimo, maendeleo ya miundombinu na italii,"amesema Reshetnikov.
 
"Maelewano ya kisiasa na kidiplomasia kati ya nchi zetu hutoa masharti mazuri ya kuimarisha biashara na mwingiliano wa kiuchumi. Kulingana na makadirio yetu, biashara kati ya nchi zetu inaweza kuongezeka maradufu,” Amesema Reshetnikov.
 
Kupitia mkutano huo Wafanyabiashara wa Tanzania wameonesha nia kubwa kwa Urusi na wafanyabiashara wa Urusi wako tayari kuingia katika masoko mapya, kuwekeza katika miradi ya pamoja na kushiriki teknolojia.