#KAZIINAONGEA
  
Katika miaka michache ijayo Watanzania wataepukana kabisa na adha ya kukatika kwa umeme kutokana na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanikiwa kuendelea  kukamilisha miradi yote ya  kuzalisha umeme nchini.

Ikumbukwe kuwa mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) umeshaanza kuzalisha umeme na hivi karibuni mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo unaosimamiwa na nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda utakamilika kwani utekelezaji wake umefikia asilimia 99.9.

Mradi huo unatarajiwa  kuzinduliwa Februari 2025 na  ma-Rais wa nchi hizo tatu wakitarajiwa kuhudhuria hafla ya uzinduzi huo.
 
 Mradi wa huo wa kufua umeme unaotokana na maji wa Rusumo, umeanza kuzalisha megawati 80 ambazo zinagawanywa kwa usawa wa megawati 26.66 kwa nchi ya Tanzania, Rwanda na Burundi na hivyo kuzidi kuimarisha gridi za Taifa za umeme.
 
Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya Umeme ya Rusumo (RPCL) inayomilikiwa na nchi zote tatu ni kielelezo cha azma ya Serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kijamii.
 
Aidha mradi huo  hadi sasa umezalisha ajira kwa zaidi ya watu 100 pamoja na kusaidia uwepo wa miradi mbalimbali kwa ajili ya huduma kwa jamii (CSR) hususan katika Halmashauri ya Ngara. 
 
Aidha, mradi huo umeiunganisha Tanzania na nchi za Rwanda na Burundi na pia unatoa fursa ya kuziuzia umeme nchi hizo endapo zitahitaji licha ya uwepo wa megawati 26.66 zinazopatikana kwa kila nchi.

#KAZIINAONGEA