TANZANIA INAONGOZA KUUZA UMEME KWA BEI NDOGO AFRIKA.
#KAZIINAONGEA
Tanzania ndio nchi pekee inaongoza kwa kuuza umeme kwa bei ndogo kuliko nchi zote za Afrika Mashariki na kuwa na Uchumi Jumuishi kwenye eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Haya ni matokeo chanya yanayotokana na jitihada zinazofanywa na Rais wa awamu ya sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha huduma hii muhimu ya Nishati ya umeme inawafikia Watanzania katika maeneo yote.
Ni ukweli uliowazi kwamba, kwa hivi sasa Serikali kupitia Wizara ya Nishati, inazalisha umeme wa ziada lakini inashindwa kuusafirisha umeme huo kwenda kwenye maeneo ndani na nje ya nchi yenye uhaba wa umeme kutokana na upungufu wa njia za kusafirisha umeme.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha PPP, David Kafulila, amesema kuwa, kutokana na changamoto hiyo, Serikali ya Tanzania imeanza mazungumzo na kampuni mbili za kigeni zenye nia ya kuwekeza jumla ya Dola za Marekani Bilioni 1.2 (Shilingi trilioni 3.2) kwenye Miradi ya kusafirisha umeme kupitia ubia wa Sekta ya umma na Sekta binafsi (PPP).
Kampuni hizo tayari zimeshaanza mazungumzo na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre) kuhusu uwekezaji huo.
Iwapo watafanikiwa, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwenye historia ya nchi kutokea uwekezaji mkubwa wa njia za kusafirisha umeme kupitia ubia PPP.
Aidha, Serikali kwa sasa inajifunza kutoka kwa nchi za Latin America na Asia zenye uzoefu mkubwa wa ushirikiano wa sekta za umma na binafsi kwenye ujenzi wa miundombinu ya umeme.
Amezitaja nchi hizo kuwa ni India, Peru, Chile, Brazil na Philippines.
Majukumu ya Kituo cha PPP ni pamoja na kuratibu na kuchambua miradi yote ya uwekezaji wa ubia kati sekta ya umma na sekta binafsi.
Tanzania inakabiliana na changamoto kadhaa kwenye eneo la ubia PPP katika miradi ya kusafirisha umeme, ikiwemo masuala ya kanuni, sheria na upungufu wa uzoefu na utaalamu husika kwenye baadhi ya taasisi za umma.
Kafulila amesema, kutokana hilo, kuna haja ya Taasisi za umma na Watumishi wa umma kujengewa uwezo ili serikali iweze kushiriki kikamilifu kwenye ubia PPP ndani ya sekta ya nishati.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa miradi ya ubia PPP kwenye ujenzi wa njia za kusafirisha umeme katika nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania, Uganda na Kenya.
Uzoefu wa wachumi wa nishati unaonesha kuwa, sekta ya nishati inaweza kujitegemea kujiendesha yenyewe kifedha iwapo bei ya umeme itapangwa kibiashara.
Wizara ya Nishati ilitangaza mwaka 2022 kuwa Serikali inahitaji Dola za Marekani Bilioni 1.9 (zaidi ya Shilingi Trilioni 5) ili kuimarisha njia za kusafirisha umeme nchini.
Amesema kuwa, ubia na PPP kwenye ujenzi wa njia za kusafirisha umeme utaleta manufaa makubwa kwenye uchumi wa Taifa.
#KAZIINAONGEA
TANZANIA INAONGOZA KUUZA UMEME KWA BEI NDOGO AFRIKA.
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 16, 2024
Rating: 5
No comments