TAIFA STARS YAMPA USHINDI RAIS SAMIA NA WATANZANIA
#KAZIINAONGEA
Ndege iliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeleta tija baada ya kikosi cha timu hiyo kuibamiza timu ya taifa ya Ethiopia bao 2-0.
Ushindi huo umeelekezwa kama zawadi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na mchango wake mkubwa kwenye mchezo huo na kwa Watanzania kwa ujumla kutokana na sapoti yao kwa Stars.
Hivi karibuni Rais Samia ambaye ni mwanamichezo, ni mpenzi wa soka na tangu aingie madarakani ameleta mapinduzi makubwa kwenye michezo mbalimbali ukiwemo soka aliamua kutoa ndege maalum ya kukipeleka kikosi hicho ili kifike nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bila bughudha.
Taifa Stars ilicheza Novemba 16,2024 dhidi ya timu ya Taifa ya Ethiopia katika mchezo wa kusaka tiketi ya fainali za AFCON 2025.
Awali Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Ali maarufu kama Hemedi Morocco alimshukuru Rais Samia kwa kutoa ndege ya Serikali kwa mara nyengine ili iwapeleke wachezaji wa Taifa Stars kwenda kulipigania taifa lao.
"Namshukuru mama yetu Rais Samia kwa kutupatia tena ndege ya kutupeleka DRC, tunaamini huu ni upendo wa hali ya juu ya Stars na kwa soka la Tanzania kwa ujumla.
"Ahadi yetu ilikuwa ni moja tu, nayo ni ushindi na tumeshinda, angalau tumejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali za AFCON 2025 zitakazochezwa Morocco."
*#KAZIINAONGEA*
TAIFA STARS YAMPA USHINDI RAIS SAMIA NA WATANZANIA
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 20, 2024
Rating: 5
No comments