#KAZIINAONGEA
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwajali wananchi na wawekezaji nchini kwa kuwarahisishia upatikanaji wa huduma ya umeme wa uhakika.

Baadhi ya wamiliki wa migodi waliopo wilayani Ulanga, mkoani Morogoro wamesema kuwa ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ifakara umepunguza gharama za uendeshaji katika migodi iliyopo wilayani humo

Mkude Msimbe ambaye ni Meneja katika Mgodi wa Ruby International Ltd amesema uwepo wa kituo hicho umupunguza gharama za uendeshaji tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo kukatika mara kwa mara kwa umeme kuliwalazimu kutumia jenereta kuendesha shughuli zao za uchimbaji.

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wamewezesha ujenzi wa kituo hicho ambao umeongeza umeme wa uhakika katika Wilaya za Ulanga, Malinyi na Ifakara.

#KAZIINAONGEA