SERIKALI YAPELEKA UMEME JUA VISIWANI ZIWA VICTORIA
KAZIINAONGEA
Nia ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kila kona ya nchi inapata umeme wa uhakika bila kujali umeme4 huo umezalishwa kwa maji, upepo ama jua.
Dhamira hiyo imeisukuma serikali kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kupanga kutumia kiasi cha tsh bilioni 2.1 kufikisha umeme wa jua katika visiwa vya Ziwa Victoria vilivyopo Wilaya ya Bukoba na Muleba Mkoani Kagera.
Mradi huo ni mpango maalumu wa kuwawezesha mwananchi kupata huduma ya umeme bila vikwazo.
Hii inamanisha kuwa serikali ya Dkt. Samia imedhamiria kuhakikisha visiwa vyote ambavyo havijafikiwa na Gridi ya Umeme wa Taifa vinapata umeme kwa chanzo kinachoweza kutoa umeme huku gharama ya asilimia 55 hadi 75 ikibebwa na serikali kulingana na ukubwa wa huduma inayotolewa kwa wananchi na wafanyabiashara walioko visiwani.
Aidha katika umeme ambao umefungwa katika kisiwa cha Musira kaya 192 zinatarajia kunufaika huku kaya 50 tayari zimeishaanza kutumia mfumo huo na maeneo yanayotoa huduma za umma kama shule na nyumba za ibada tayari nao wameanza kutumia mfumo huo.
Ileleweke kuwa mikoa saba ya Tanzania, wilaya 16 na kata 43 pamoja na visiwa 118 nchini vitanufaika na umeme jua kwa gharama ya Sh bilioni 8.
#KAZIINAONGEA
SERIKALI YAPELEKA UMEME JUA VISIWANI ZIWA VICTORIA
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 20, 2024
Rating: 5
No comments