SERIKALI YAJIPANGA KUWA NA UCHAGUZI WA HAKI, UWAZI NA KUZINGATIA KANUNI.
#KAZIINAONGEA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha kuwa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mtaa, unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, unafanyika kwa uwazi, haki na kwa kuzingatia kanuni zilizowekwa.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni muhimu kwa kuimarisha Demokrasia na ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi yanayowahusu ambapo katika uchaguzi huu, jumla ya nafasi 332,584 zitagombewa.
Rais wa awamu ya sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mikutano yake mbalimbali nchini, amekuwa akiwasihi Watanzania kutopuuzia Uchaguzi wa Serikali na kuwataka watumie fursa hiyo kugombea na kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kila baada ya miaka mitano, wananchi wanapata fursa ya kuchagua viongozi wanaowakilisha maslahi yao katika ngazi za chini za Serikali na Uchaguzi huo hufanyika kila baada ya miaka mitano, uchaguzi wa mwisho wa Serikali za Mitaa ulifanyika mwezi Novemba mwaka, 2019.
Aidha, uongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji,Vitongoji ndio msingi wa uongozi katika nchi, hivyo ni vyema kuchagua viongozi bora ili kujenga msingi imara.
#KAZIINAONGEA
SERIKALI YAJIPANGA KUWA NA UCHAGUZI WA HAKI, UWAZI NA KUZINGATIA KANUNI.
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 20, 2024
Rating: 5
No comments