#KAZIINAONGEA

Afya ni mtaji hivyo ndivyo unavyoweza kusema na ukweli wa hilo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaujua na ndio maana ameridhia serikali yake kutoa kiasi cha  Tsh 100 milioni kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Nyasaungu, kilichopo katika jimbo la Musoma vijijini mkoani Mara.

Kijiji cha Nyasaungu kina  vitongoji vitano na kwa sasa  kinakamilisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutoa huduma za Afya  Disemba 1, 2024

Nyasaungu  ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu kikiwa pamoja na kijiji cha  Kabegi na Kiemba ambavyo kila kimoja kina zahanati yake.

Kukamilika kwa Zahanati hiyo kutavifanya vijiji vya Kata ya Ifulifu kila kimoja kuwa na  zahanati yake.

Mbali na fedha kutoka serikalini, lakini pia wananchi kwa umoja wao wamechangia fedha na nguvu kazi kwa kushirikiana na mbunge wao Profesa Sospeter Muhongo.

Jengo kuu la Zahanati hiyo  liko katika hatua za mwisho kabisa za kukamilika, choo chenye matundu matatu kinajengwa na muda wa ujenzi unapaswa kuisha Novemba 30,mwaka huu.

#KAZIINAONGEA