Home
/
Unlabelled
/
SERIKALI YA RAIS DKT. SAMIA YAWEKEZA BILIONI 60 MABORESHO YA BANDARI ZIWA VICTORIA, ni Bandari za Mwanza, Kemondo na Bukoba
SERIKALI YA RAIS DKT. SAMIA YAWEKEZA BILIONI 60 MABORESHO YA BANDARI ZIWA VICTORIA, ni Bandari za Mwanza, Kemondo na Bukoba
#KAZIINAONGEA
Mafanikio katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, yameonekana wazi katika nyanja zote, na hii inaonyesha jitihada zinazofanywa na Rais katika kuliletea Taifa maendeleo.
Rais Dkt. Samia amefanya makubwa mengi ikiwa katika Sekta ya Uwekezaji, Bandari, Miundombinu ya Barabara, Reli, Maji, Afya, Elimu pamoja na maeneo mengine, na hivyo kuvutia Wawekezaji kuja kuwekeza nchini na kutoa fursa za ajira kwa Watanzania.
Kwa kuendelea kufanya maboresho katika Bandari hapa nchini, Serikali ya awamu ya sita, imewekeza nguvu zake kwa kufanya maboresho makubwa katika Bandari za Mwanza, Kemondo, na Bukoba.
Maboresho haya katika Bandari hizi, yameigharimu Serikali ya Tanzania Shilingi Bilioni 60 ambazo zitatumika katika kuboresha kina cha maji, kuongeza urefu wa gati, na kuimarisha miundombinu ya kisasa kama maeneo ya abiria, vituo vya ukaguzi wa mizigo, na mifumo ya usalama.
Maboresho haya yataleta mabadiliko makubwa katika muonekano mzima wa Bandari hizi, mabadiliko katika usafiri, usafirishaji, na uchumi wa kanda ya Ziwa Victoria na Taifa kwa ujumla, lakini pia yatarahisisha shughuli mbalimbali kufanyika kwa urahisi.
Kwa mwaka jana walifanikiwa kukusanya Bilioni 8 kwa upande wa abiria peke yake, hivyo kufanyika kwa maboresho hayo kutaiongezea Serikali Mapato lakini pia kumewapa matumaini makubwa kibiashara Wananchi wa Kanda ya Ziwa katika Uongozi wa Rais Dkt. Samia.
Maboresho haya makubwa katika Bandari za Mwanza, Kemondo, na Bukoba yanaendelea kufanyika ambapo katika Bandari ya Bukoba maboresho yamefanyika kwa asilimia 75, Bandari ya Kemondo tayari yamefanyika kwa zaidi ya asilimia 90, na Bandari ya Mwanza Kaskazini asilimia 44.
Wakili Erasto Lugenge Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, anasimamia kukamilika kwa mradi huu ambao utafanikisha kuanza kwa safari za Meli ya Mv. Mwanza, ambayo inauwezo wa kubeba abiria 1200 ukilinganisha na Meli ya sasa inayobeba abiria 600.
Maboresho haya yataongeza mapato kwa Taifa ambapo kwa mwaka 2023 Serikali iliweka lengo la ukusanyaji mapato wa Shilingi Bilioni 4.2 lakini badala yake walifanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 4 kamili.
Kukamilika kwa maboresho haya kutainufaisha Serikali kwa kuweza kukusanya mapato ya Shilingi Bilioni 8 kwa kubeba abiria tu pia kutarahisisha shughuli za uchukuzi baina ya bandari hiyo, Mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi Jirani zinazunguka mikoa hiyo.
#KAZIINAONGEA
SERIKALI YA RAIS DKT. SAMIA YAWEKEZA BILIONI 60 MABORESHO YA BANDARI ZIWA VICTORIA, ni Bandari za Mwanza, Kemondo na Bukoba
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 20, 2024
Rating: 5
No comments