#KAZIINAONGEA

Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeanza mchakato wa kuanzisha Programu ya Taifa ya Lishe baada ya  Serikali kuifuta Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC).

Mchakato huu wa Serikali umekuja kufuatia kuibuka kwa hoja kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Alice Karungi Kaijage aliyehoji  kama kuna haja ya Serikali  kuhuisha Taasisi ya Lishe badala ya kuifuta kabisa.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameeleza Bungeni kuwa, Wizara ya Afya inatarajia kuanzisha Programu ya Taifa ya Lishe pamoja na kuanzisha Kitengo cha Utafiti wa Lishe katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). 

Kutokana na kuanzishwa kwa programuhiyo, Seriakali imeona kuna haja ya majukumu yote yaliyokuwa yanatekelezwa na TFNC kufanywa kwa upana wake na Programu ya Taifa ya Lishe.

Tamko la kufutwa kwa TFNC lilitolewa na Msajili wa Hazina  Desemba 15, 2023 na kwamba majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na taasisi hiyo sasa yatahamishiwa kwenye Programu ya Taifa ya Lishe pamoja na kitengo kipya cha utafiti wa lishe ndani ya Taasisi ya NIMR.

Hatua za awali za kuanzisha programu hiyo tayari zimeanza, hatua inayolenga kuboresha masuala ya lishe na utafiti wa kisayansi nchini.

# KAZIINAONGEA