SERIKALI YA DKT. SAMIA YAFANYA MKUTANO WA UVUVI ENDELEVU NA UCHUMI WA BULUU
#KAZIINAONGEA
Tanzania ni moja ya nchi Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo inaweka mikakati ya namna ya kudhibiti mabadiliko ya Tabia nchi kwa uvuvi endelevu mazao ya uvuvi yaliyopo katika Bahari ya Hindi.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi mahiri wa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kufanya mikakati mbalimbali katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi, pamoja na kuweka jihada katika Uwekezaji wa Uchumi wa Buluu.
Katika kufanikisha hilo, Serikali imefanya Mkutano wa Pembezoni ukiwa na agenda inayohusu uvuvi endelevu na Uchumi wa Buluu, lengo likiwa ni kupata fursa mbalimbali za Uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi na juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.
Mkutano huo ulifunguliwa na kuongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais. Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
Amebainisha kuwa, mkutano huo umeangalia namna nchi hizo zinavyoweza kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi kwa kuvua kiendelevu na kutoharibu mazingira, hali inayoweza kusababisha mabadiliko ya tabia nchi na kusababisha madhara katika sekta ya uvuvi.
Mkutano huo umejadili mambo mbalimbali kuhusu Uwekezaji wa Uchumi wa Buluu katika nchi ambazo zinazunguka Bahari ya Hindi na Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo amefafanua kuwa uwekezaji bado ni tatizo hasa rasilimali fedha kwa nchi zinazoendelea.
Pia mkutano huo umeangalia uvunaji wa rasilimali za mazao ya uvuvi katika Bahari ya Hindi kiendelevu pamoja na kudhibiti uvuvi haramu kwa kuweka mikakati mbalimbali ili uchumi wa Buluu uwe na manufaa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Madalla amesema, Serikali ina mpango mkubwa wa kujenga vituo vya ukuzaji viumbe maji katika Ukanda wa Pwani pamoja na vituo vingine ili kufungua fursa ya uchumi wa Bahari katika ukuzaji viumbe maji.
*#KAZIINAONGEA*
SERIKALI YA DKT. SAMIA YAFANYA MKUTANO WA UVUVI ENDELEVU NA UCHUMI WA BULUU
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 16, 2024
Rating: 5
No comments