SERIKALI YA DKT. SAMIA YAFANIKIWA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MAAMBUKIZI YA HIV
#KAZIINAONGEA#
Katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwa mwaka 2024, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi Mahiri wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikiwa katika mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo, kutoka 1,700,000 mwaka 2017 hadi kufikia 1,540,000 mwaka 2023.
Mafanikio ya kupungua kwa maambukizi ya VVU yametokana na jitihada za Rais Dkt. Samia aliyewezesha kufikia mafanikio haya ikiwemo kuhakisha huduma bora za tiba na matunzo kwa WAVIU.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderianaga ameeleza kuwa, Tanzania imepiga hatua katika mapambano dhidi ya UKIMWI kufuatia kupungua kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), na hivyo kufikia idadi hiyo.
Maambukizi wa Virusi vya Ukimwi yameonekana kuathiri zaidi makundi kadhaa yakiwemo makundi ya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24, madereva wa masafa marefu, wachimbaji wadogo wa madini na wavuvi kuchangia maambukizi mapya ya ugonjwa huo hapa nchini.
Nderianaga ameyasema hayo Jijini Dodoma, kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwa mwaka 2024, ambayo Kitaifa yatafanyika Desemba 1, 2024 Mkoani Ruvuma.
Utafiti wa hali ya UKIMWI nchini (Tanzania HIV Impact Survey) kwa mwaka 2022/23, umeonyesha Mikoa mitatu yenye kiwango cha juu cha maambukizi ni Njombe asilimia 12.7, Iringa asilimia 11.1 na Mbeya asilimia 9.6, na Mikoa yenye maambukizi ya chini ni Kigoma asilimian 1.7, Manyara asilimia 1.8 na Lindi asilimia 2.6.
Tanzania imepiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali za mwitikio wa VVU ambapo kwa mujibu wa ripoti ya UNAIDS 2022, Tanzania imefikia Mkakati wa Kimataifa wa UKIMWI 2021 hadi 2026 kwa lengo la matibabu.
Mafanikio haya yamechangiwa na matokeo ya Utafiti wa Athari za VVU Tanzania Mwaka 2022-2023 ambao uliripoti kufikiwa kwa malengo ya UNAIDS 95-95-95 kwa asilimia 82.7, asilimia 97.9 na asilimia 94.3 (ngazi ya jamii).
#KAZIINAONGEA
SERIKALI YA DKT. SAMIA YAFANIKIWA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MAAMBUKIZI YA HIV
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 20, 2024
Rating: 5
No comments