*●Ndio Sekta inayoongoza kuingiza fedha nyingi za kigeni nchini*

#KAZIINAONGEA

Katika kipindi cha miaka mitatu tangu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, ameweza kuifanya Sekta ya Madini kuwa Sekta kiongozi kwa kuliingizia Taifa fedha nyingi za kigeni, na hivyo kufanya mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa kuongezeka kutoka asilimia 4.4 mwaka 2017 hadi asilimia 9.1 mwaka 2022.

Maingizo haya ya fedha za kigeni yameifanya Sekta ya Madini kuwa Sekta kiongozi kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni ambapo Mauzo ya bidhaa nje ya nchi yalikuwa Dola za Marekani Bilioni 3.1 sawa na asilimia 56 ya fedha yote ya kigeni iliyopatikana hapa nchini, na mafanikio hayo ya madini yalipatikana katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Mafanikio kwenye Sekta ya Madini kwa upande wa suala la usalama kwenye migodi haliwezi kuachwa nyuma, na katika kutambua hilo Tume ya Madini kupitia Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira imekuwa ikifanya kaguzi za mara kwa mara kwenye migodi ya madini pamoja na kutoa elimu.

Mbali na mafanikio hayo pia mengine ni pamoja na ongezeko la utoaji wa leseni za madini kutoka leseni 5094 katika mwaka wa fedha 2018/2019 hadi leseni 9642 katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Kazi hii kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza fursa zilizopo nchini, imewezesha kampuni nyingi za kigeni, kuendelea kuonyesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini hapa nchini.

Sekta hii imekuwa ikisimamiwa kwa ukaribu na Serikali na hii ni kutokana na umuhimu na unyeti wake katika Taifa, hasa ukizingatia kuwa ndio inayoongoza kwa kukuza pato la Taifa.

Kutokana na unyeti huo, Sekta ya madini imekuwa ikifanya mkutano wake wa mwaka ambapo kwa mwaka 2024, u?meanza Novemba 19- 21, huu ni Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Ni mkutano unaotumika kutangaza fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Madini ikihusisha watoa mada kutoka ndani na nje. 

#KAZIINAONGEA