SERIKALI IMEANZA KUTEKELEZA UJENZI KITUO CHA KUPOZA UMEME SIMIYU
#KAZIINAONGEA
Katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imeanza kutekeleza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katika eneo la Imalilo, Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kwa kujenga line ya umeme kutoka kwenye kituo hicho hadi Meatu.
Hii ni muendelezo wa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kukabiliana na tatizo la umeme ikiwa ni pamoja na kufungwa vidhibiti umeme katika njia ya awali, kujenga njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkalama Mkoani Singida hadi Bukundi Wilayani Meatu, sambamba na zoezi la kubadilisha nguzo zilizochakaa na kuweka nguzo za zege.
Kukatika kwa umeme Wilayani Meatu, kunatokana na umbali mrefu wa njia ya kisafirisha umeme pamoja na uchakavu wa miundombinu ya umeme.
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, ameyasema hayo Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Liwale Zuberi Kachauka, kuhusiana na uamuzi wa Serikali kuejenga kituo cha umeme Jimbo la Liwale.
Kuhusiana na mradi wa umeme Mtwara, amesema Serikali inatekeleza mradi huo kwa kuunganisha Mikoa ya Mtwara na Lindi na umeme wa gridi kutokea Songea kwa kupitia njia ya Tunduru, Masasi-Mahumbika.
Kujengwa kwa Kituo cha umeme Liwale, kutasaidia kuboresha upatikanaji wa umeme Liwale ambapo kwa sasa Serikali inatekeleza Mradi mkubwa wa kupeleka umeme gridi ya Taifa kwa mikoa hiyo.
Suala malipo ya fidia ya wananchi wa Namtumbo waliopita mradi wa gridi ya Taifa kwenda Mikoa ya Mtwara na Lindi, Kapinga amesema, agizo la Rais Dkt. Samia ni kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fidia.
Wananchi wa maeneo husika, wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kupisha maeneo yao ili mradi uweze kukamilika kwa wakati kwa manufaa ya Taifa.
#KAZIINAONGEA
SERIKALI IMEANZA KUTEKELEZA UJENZI KITUO CHA KUPOZA UMEME SIMIYU
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 06, 2024
Rating: 5
No comments