#KAZIINAONGEA
 
Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2024, miradi 354 kati ya miradi 998 ya maji iliyopokea fedha kutoka Mfuko wa Taifa wa Maji katika maeneo mbalimbali ya nchi  imekamilishwa na  kuwanufaisha wananchi takribani milioni 5.3.

Miradi hiyo ambayo inasimamiwa na Serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu imesaidia kupeleka  huduma bora za maji katika maeneo ambayo awali yalikosa huduma ya uhakika ya maji.
 
Aidha serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji imeendelea kutekeleza miradi ya uhifadhi wa vyanzo vya maji ambapo takribani miradi 104 ya uhifadhi na uendelezaji wa vyanzo vya maji imetekelezwa.
 
Serikali itaendelea kusimamia miundombinu ya maji ili kuzuia upotevu pamoja na wizi wa maji ili kuwezesha huduma hizo kuwafikia wananchi kwa ufanisi zaidi.