RAIS SAMIA AFANIKISHA UTALII TIBA TANZANIA
#KAZIINAONGEA
Ni mwanamke wa shoka, ni mama ni bibi na ni mlezi wa kweli wa Watanzania wote bila kujali itikadi ama rangi zao, yeye ndie aliyebeba dira ya Mtanzania na Tanzania kwa ujumla.
Ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambae Askofu Dkt. Fredrick Shoo hivi karibuni alinukuliwa akikiri kuwa kiongozi huyu ni chaguo la Mungu anaestahili kuongoza sasa na hata baada ya sasa.
Rais Samia kiongozi mbeba maono amefanikiwa kuipaisha Tanzania kiutalii, uamuzi wake wa kushiriki filamu ya Royal Tour ulitosha kuonesha mwanamama huyo amedhamiria nini kwa nchi yake.
Royar Tour imelipa, watalii wanapishana huku na kule kutembelea vivutio vyetu vya utalii nchini.
Sasa amehamishia nguvu kwenye utalii wa Tiba, na serikali yake imezichagua hospitali maalum ambazo zitaendesha mpango wa utalii wa kimatibabu (Utalii tiba).
Hospitali hizo ni Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).
Kwakuwa dhamira ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba kwa nchi za Afrika Mashariki na ikiwezekana Afrika kwa ujumla, uwekezaji katika utalii wa matibabu utakuwa endelevu na hospitali za rufaa zitajengwa katika kanda zote nchini na mipango iko tayari kuwa na kituo kingine kikubwa cha rufaa mkoani Kigoma kitakachotoa huduma za matibabu ikiwemo utalii wa matibabu.
Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu ya matibabu, kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya katika ngazi za madaktari bingwa.
#KAZIINAONGEA
RAIS SAMIA AFANIKISHA UTALII TIBA TANZANIA
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 16, 2024
Rating: 5
No comments