Home
/
Unlabelled
/
RAIS DKT. SAMIA AFANIKISHA MATENGENEZO YA MABEHEWA 264 NCHINI CHINA, TRC kuanza kusafirisha mizigo kwa Reli ya SGR February, 2025
RAIS DKT. SAMIA AFANIKISHA MATENGENEZO YA MABEHEWA 264 NCHINI CHINA, TRC kuanza kusafirisha mizigo kwa Reli ya SGR February, 2025
#KAZIINAONGEA
Jitihada zinazoendelea kufanywa tangu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, zinaonekana ambapo Rais amepambana kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inakamilika ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zinalikabili Taifa kwa kipindi kirefu.
Pamoja na kuwepo miradi mingi mikubwa iliyoigharimu Serikali kiasi kikubwa cha fedha lakini pia, Mradi wa Treni za SGR umeonekana kuwa mkombozi kwa Watanzania katika sekta ya usafiri.
Katika kuhakikisha usafiri wa Treni ya SGR unafanikiwa ikiwa ni kwa kuwepo mabehewa ya kutosha ya abiria na ya mizigo, Serikali ya Tanzania inatarajia kupokea jumla ya shehena ya Mabehewa 264 ya mizigo kutoka nchini China, Desemba, 2024 yaliyokuwa yanafanyiwa matengenezo na Kampuni ya CRRC.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema, utengenezaji wa mabehewa hayo 264 ya mizigo umekamilika nchini China na kwamba, Meli iliyobeba mabehewa hayo imeng'oa nanga nchini humo Novemba 12, 2024 na inatarajiwa kufika Tanzania katikati ya mwezi Desemba 2024.
Katika mzigo huo kuna mabehewa 200 ya kubeba makasha (makontena) na mabehewa 64 ya kubeba mizigo isiyofungwa (loose cargoes).
Shehena hiyo ya mabehewa 264 ni sehemu ya jumla ya mabehewa 1,430 ambayo kwa mujibu wa mkataba kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya Kimataifa ya China (CRRC) yatapelekwa kwenye Reli ya kisasa ya SGR.
TRC inategemea kuanza kusafirisha mizigo kwa reli ya SGR kati ya January au February mwakani.
Akizungumzia mafanikio ya mradi huo hasa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema, kuna mafanikio makubwa kupitia mradi huo ambao hadi sasa umetumia fedha nyingi katika utekelezaji wake.
Amesema, mradi huu utafungua uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa, kwa kutambua hilo, ndiyo maana Rais Dkt.Samia amekuwa anatafuta fedha na kuzielekeza katika mradi, lengo ni kuleta maendeleo ya wananchi na kuinua uchumi wa nchi.
Pia kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi kwa nchi tunazopakana nazo ambazo hazina bandari na zinategemea bandari za hapa nchini kwa ajili ya uagizaji na usafirishaji wa mizigo yao kutoka nje, kama Reli ya kwenda Mwanza ambayo inalenga soko la Uganda.
Kuwapo kwa usafiri huo kutaiwezesha Uganda kupata mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu.
*#KAZIINAONGEA*
RAIS DKT. SAMIA AFANIKISHA MATENGENEZO YA MABEHEWA 264 NCHINI CHINA, TRC kuanza kusafirisha mizigo kwa Reli ya SGR February, 2025
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 16, 2024
Rating: 5
No comments