Mradi wa PPP wakaguliwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ofisi ya Rais TAMISEMI
Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Kituo cha Ubia baina ya sekta ya umma na binafsi-PPP, David Kafulila ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI kwa kuisimamia serikali kupitia Kituo hicho cha PPP na kusema yote yaliyoshauriwa na kamati hiyo wameyapokea na watayafanyia kazi.
Mbali na Shukrani hizo alizozitoa jijini Dar es salaam wakati wa hitimisho la ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Kafulila, amesema kituo cha PPP kikitumiwa ipasavyo kitasaidia kuchochea maendeleo na kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuongeza mapato ya Halmashauri nchini.
Kamati hiyo ya Bunge ya TAMISEMI ilitembelea mradi wa ujenzi wa kitega uchumi kwa ubia na mwekezaji binafsi Kampuni ya Tosh Logistics Limited na Shirika la Uchumi na Maendeleo la Jiji la Dar es salaam-DDC.
Mradi huo wa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 36.7 upo kwenye eneo la DDC-Kariakoo.
No comments