Breaking News

GHOROFA LAPOROMOKA KARIAKOO, RAIS ATOA MAAGIZO


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mpaka Sasa limefanikiwa kuwaokoa watu nane ambao walikwama kwenye jengo lililoanguka Kariakoo na tayari wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Zoezi la uokoaji linaendelea kwa kuwakwamua watu ambao wamekwama katika ghorofa ya chini.
Kupitia mitandao ya kijamii Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameandika ujumbe ufuatao:

"Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam. 

Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi. 

Wakati hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii."



from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/OUHQFlK

No comments