BAJETI YA 2023/24 KUJENGA SHULE 302
#KAZI INAONGEA
Moja ya mambo ambayo yanaweza kuitoa nchi kwenye umasikini ni kupambana na ujinga kwa kuhakikisha wananchi wengi wanakwenda shule.
Kwa kuliona hilo serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza programu ya elimu ya awali, Elimu msingi na Sekondari bila ada.
Katika kufanikisha program hiyo serikali ya Rais Samia imetenga kiasi cha shilingi trilioni 1.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na programu za ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule za msingi ikiwemo shule mpya 302, vyumba vya madarasa 3,880, mabweni 63 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu, matundu ya vyoo 22,418 na uzio wa mabweni katika shule 88; ukarabati wa madarasa 627 katika shule kongwe za msingi na ukamilishaji wa mabweni saba (7).
Kwa upande wa elimu ya Sekondari, Serikali tayari imejenga shule mpya 25, madarasa 6,648, mabweni 444 na matundu ya vyoo 16,795. Pia, imekarabati shule kongwe za sekondari 32, umaliziaji wa maboma ya madarasa 2,441, shule za bweni tisa (9), maabara 132 na matundu ya vyoo 1,650.
*#KAZIINAONGEA*
BAJETI YA 2023/24 KUJENGA SHULE 302
Reviewed by Tanzania Yetu
on
November 20, 2024
Rating: 5
No comments