Breaking News

WAZIRI CHANA AFUNGA ONESHO LA S!TE 2024, aeleza mafanikio



Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amefunga Onesho la Nane la Utalii la Kimataifa la Swahili (8th edition of the Swahili International Tourism Expo–S!TE 2024) lililokuwa linafanyika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kufunga Onesho hio leo Oktoba 13, 2024 Waziri Bolozi Dkt. Chana amebainisha mafanikio ikiwemo kupatikana kwa wanunuzi wa bidhaa za utalii 120.

Amesema mwitikio mkubwa katika Onesho la mwaka huu ni kwa sababu ya kufunguka Kwa Sekta ya Utalii kutokana na hamasa iliyotolewa na Rais Dkt. Samia kupitia filamu ya The Royal Toure.

"Katika Onesho la mwaka huu tumepata wanununuzi wa Kimataifa wa bidhaa za utalii takeibani 120," amesema na kuongeza,

“Sekta ya Utalii imechangia asilimia 17 ya Pato la Taifa, na pia imeingiza asilimia 25 ya fedha za kigeni,".

Waziri Balozi Dkt. Chana amebainisha kuwa watalii wameomgezeka nchini jambo ambalo linaongeza faida kiuchumi kwani Shirika la Ndege linafaidika pamoja na wananchi wanaowapokea watalii.

Aidha amesema Ulinzi wa rasilimali za Tanzania ikiwemo Misitu na mbuga ni muhimu sana Kwa Taifa na kipaumbele kwa kila mtu ili kuendelea kustawisha uchumi wa nchi hivyo watanzania wanapaswa kuzitunza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania,Balozi Dkt. Ramadhan Dau amesema mafanikio waliyopata Kwa mwaka huu ni ishara tosha ya mafanikio ya maandalizi ya Onesho lijalo ambapo Kwa mwaka huu limefanyika Kwa mara ya nane tangu lilipoanzishwa mnamo mwaka 2014.


No comments