Tuzo ya Usiku wa Madini 2023 yampa hamasa kuanzisha kampuni, kutoka kuuza maandazi hadi kumiliki leseni 95 za madini
Kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2024,
TUZO YA USIKU WA MADINI 2023 YAMPA HAMASA KUANZISHA KAMPUNI
Kutoka Kuuza
Maandazi hadi kumiliki Leseni 95 za Madini ya Bati (Tin) Moja ya Dhahabu
Tuzo hiyo ilimpa hamasa kubwa ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini na sasa ameanzisha kampuni inayojulikana kama Rare Mining East Africa LTD yenye jumla ya leseni 21 za uchimbaji mdogo wa Madini ya bati na leseni 74 zipo kwa jina lake.
Ili kupata
leseni hizo, ilimlazimu Bi. Leminatha kulipa kiasi cha shilingi milioni 150
Serikalini ikiwa ni ada za leseni baada ya wamiliki wa awali kushindwa
kuzilipia na kuziendeleza. Pia, alilipia leseni 33 za mdaiwa mwingine kwa kiasi
cha shilingi milioni 120 na kuziendeleza. Kwa kifupi ni kwamba hivi sasa
mwanamama huyu anamiliki jumla ya leseni 95 za uchimbaji mdogo wa madini ya
bati (Tin) na 1 ya dhahabu zote zikiwa hai na zinaendelezwa.
‘’ Ile tuzo
ilinipa hamasa kubwa na nguvu za kusonga mbele zaidi, nilijishukuru mwenyewe
kwanza, kwa kutokukata tamaa. Sikuwa na kampuni lakini sasa hivi nina kampuni
yangu na ina leseni 21 za uchimbaji wa
madini ya bati. Nimehamasisha watu kulipa madeni ya Serikali zaidi ya shilingi
milioni 300 waliokuwa wadaiwa sugu. Furaha yangu ni kwamba nilianzia chini sana
kuelekea juu, maana nilianza kwa kuuza maziwa na mandazi, baada ya kufiwa na
mzazi mwenzangu, sikupewa chochote, lakini nilisonga mbele kwa sababu nilikuwa
na picha kubwa. Ile tuzo imefanya nianzishe NGO’s na kuanza kuishi maisha ya
mguso katika jamii yangu,’’ anasema Leminatha.
Leminatha
alitunukiwa tuzo hiyo katika hafla ya Usiku wa Madini inayofanyika kila mwaka
wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania.
Usiku wa Madini umekuwa ukitumika kama sehemu ya kutambua mchango wa wadau
mbalimbali waliofanya vizuri katika Sekta ya Madini kupitia vipengele
mbalimbali kama uchangiaji bora wa mapato kwa Serikali, uwajibikaji wa kampuni
kwa jamii, ushirikishaji watanzania, uongezaji thamani madini ambayo kwa pamoja
yamechangia katika ukuaji na maendeleo
ya sekta ya madini nchini.
Pia, Usiku huo huenda sambamba na onesho
maalum la madini ya vito na usonara linalolenga kutangaza fursa za uwekezaji
zilizopo kwenye madini ya vito pamoja na kuhamasisha matumizi ya bidhaa za
mapambo zinazotengenezwa nchini.
Akielezea
historia yake ya uchimbaji, Leminatha anasema alianza shughuli zake mwaka 2017
katika kijiji cha Mwime, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ambapo alikuwa
akichimba na kukusanya madini ya dhahabu. Mnamo mwaka 2021 alielekeza shughuli
zake Mkoani Kagera Wilaya ya Kyerwa ambapo anachimba madini ya bati (Tin)
katika leseni zake na kuuza kwa wafanyabiashara wakubwa (dealers) kupitia Soko
la Madini Kyerwa. Anaongeza kwamba amejielekeza
kwenye madini ya bati kutokana na mahitaji ya madini hayo duniani hivi sasa
yanauzika bila kikwazo.
‘’
Kilichonisukuma kuwekeza sekta ya madini ni kwa sababu mimi mwenyewe ninapenda
madini hivyo niliamini ninaweza kufanikiwa katika sekta ya madini. Ninafanikiwa kwa sababu ya Sera na Sheria
rafiki katika sekta ya madini. Pia ninapata ushauri sahihi kutoka kwa viongozi
wa Serikali ambao wanaonishauri vyema na kupata mafanikio. Kwa ujumla
ninafurahia uwekezaji wangu kwenye Sekta ya Madini kutokana na namna serikali
inavyotuongoza vema,’’ anasema Leminatha.
‘’Kwanza
ninapenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, ninaishukuru Serikali kwa kutambua
nafasi ya kila mchimbaji hususan sisi wanawake. Ninamshukuru Rais wangu Mhe.
Samia Suluhu Hassan, kwangu mimi siyo Rais tu bali ni mwalimu na darasa
linaloishi, ninawashukuru Maafisa Madini wote na hususan Samwel Shoo kwa
kuniamini na kunisaidia kupata leseni za madini na sasa nina jumla ya leseni 95
zote zikiwa zinafanya kazi,’’ anaongeza Leminatha.
Leminatha
anapenda kuwaasa wanawake wengine kutambua kwamba kazi ni muhimu na inaongeza
thamani ya mwanamke na ana amini kuwa mwanamke ni mzalishaji mzuri kutokana na
nguvu aliyonayo pindi anaporuhusu ifanye
kazi, ‘’ mwanamke nakushauri fanya lolote kwa moyo wa kupenda na tafuta maarifa
kwenye hilo eneo, nakuhakikishia matafanikio yatakutafuta, hutoyatafuta na
ukifanya kazi utaleta suluhu na mafanikio makubwa kwenye familia yako. Tambua
watoto wanajifunza kwetu sana kuliko kwa baba zao, je wanajifunza nini kwako
kama mama,’’? anaeleza.
Akizungumzia
changamoto za uwekezaji wake anasema zipo na hazikosekani na kuzitaja kuwa ni
pamoja na kupanda na kushuka kwa bei za madini hayo, hata hivyo Leminatha
anasema changamoto hiyo inampa ari ya kusonga mbele kwasababu anapenda kufanya
kazi na kujituma ili kuacha alama katika vizazi vijavyo, ‘’sipendi kubweteka,
uwajibikaji unanipa nguvu ya kujivunia kuzaliwa Tanzania, na kubwa kabisa ni
furaha yangu pale ninapochangia pato la nchi yangu,’’ anasema Leminatha.
Akizungumzia
mipango yake siku za usoni anasema ni kusafirisha madini kwenda soko la dunia
na baadaye kujenga viwanda vyake hapa nchini na kutumia madini kutengeneza
bidhaa mbalimbali za madini yanayozalishwa nchini zenye nembo yake ya LEM-NES
INTERNATIONAL LTD, na kuongeza naamini hili litatamia,’’.
Mwaka 2020
Tanzania ilijiunga na mpango wa Nchi za Maziwa Makuu wa
kuhakikisha madini ya 3Ts yaani (tin – bati, tantalum na walfranite)
yanazalishwa kwenye vyanzo visivyo na migogoro ya kivita na vinavyokidhi
viwango vya chini vya kijamii (mfano: hakuna watoto wanaofanya kazi) maarufu
kama ICGLR. Kutokana na Tanzania kujiunga kwenye mfumo huo (ICGLR) wachimbaji
wa Tin wamepata fursa ya kuuza madini ya Tin nchi yoyote duniani na kupata uhakika wa masoko kutokana na cheti
hicho cha ICGLR kuyatambulisha rasmi.
Soko la
madini ya Tin lilizinduliwa mwezi Mei, 2019 mkoani Kagera Wilaya ya Kyerwa.
Madini ya bati yana matumizi mbalimbali ikiwemo kutumika kuunganisha vitu
mbalimbali kama mabomba ya chuma na metali (Steel/ Metal), mifumo ya umeme
(electric circuit), mifumo ya kielektroniki ya simu, vyuma vya reli, mifumo ya
ndege na mifumo ya lifti za umeme kwenye ghorofa.
Pia, madini
ya hayo hutumika kuzuia kutu kwenye
vyombo vya kuhifadhia chakula (Tin plated steel containers au Tin cans food
storage containers) kwa muungano wa madini ya chuma. Tin vilevile hutumika
kuzuia kutu kwenye mabati ya kujengea nyumba (Iron sheet tin coating).
Leminatha
amekuwa mwanamke wa mfano kati ya wengi waliowekeza katika mnyororo wa shughuli
mbalimbali za madini. Ili kuhakikisha
wanawake wengi zaidi na vijana wanashiriki katika uchumi wa madini, katika
Mwaka wa Fedha 2024/25, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeandaa program
maalum ya Mining For Brighter Tomorrow (MBT) inayolenga kuwaendeleza vijana na
wanawake wachimbaji kwa kuwapatia
leseni za maeneo ya kuchimba, vifaa, magari na mitambo.
#TMIC2024
#
TanzaniaMiningAnd Investment Conference
#Value
Addition for Socio-Economic Development
#UongezajiThamaniMadinikwa
Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi
Mkutanowa
Kimataifa wa Uwekezaji katikaSekta ya Madini Tanzania2024
No comments