TUNAIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA MIUNDOMBINU YA NISHATI ILI KUFIKISHA HUDUMA KWA WOTE- DKT.MATARAGIO
*Asisitiza nia ya Serikali ni kutoa huduma stahiki bila kuangalia umbali au kipato*
*Apongeza kampuni ya Puma Energy Tanzania kushirikiana na Serikali uhamasishaji Nishati Safi ya Kupikia*
*Puma Energy Tanzania yaahidi kuendeleza ushirikiano*
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema Serikali
inaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na miundombinu ya Sekta ya
Nishati nchini ili kuwezesha wananchi kufikiwa na huduma stahiki bila
kujali umbali na vipato vyao.
Dkt.
Mataragio ameyaeleza hayo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya
utoaji Tuzo kwa Mawakala na Wadau wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania
ambayo inaunga mkono juhudi za Serikali za kuelimisha jamii kuhusu
matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia bidhaa za Puma Gas.
Dkt.
Mataragio amesema moja ya majukumu ya Wizara ya Nishati ni kukutana na
wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma na watumiaji ili kuimarisha
ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali utakaopelekea utoaji wa
huduma bora kwa wananchi ikiwa ni moja ya vipaumbele vya Serikali.
Katika
hafla hiyo, Dkt.Mataragio ameipongeza kampuni ya Puma kwa jitihada
zinazounga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuhamasisha
jamii ili itumie Nishati Safi ya Kupikia na hivyo kutimiza lengo la
asilimia 80 ya Watanzania kutumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo mwaka
2034.
Amesema
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
amekuwa Balozi na kinara katika kuhamasisha matumizi ya Nshati Safi ya
Kupikia nchini na Duniani ili kuhakikisha Watu wanaondokana na matumizi
ya kuni na mkaa ambao una madhara kwa afya na kusababisha uharibifu wa
mazingira.
Kuhusu
Tuzo hizo zilizotolewa na Puma Energy Tanzania kwa Mawakala na Wadau
mbalimbali nchini, Dkt.Mataragio ameelekeza kuwa ziwe chachu ya
kuendelea kufanya kazi kwa weledi na ufanisi kulingana na vigezo na
mashariti ya Kampuni kwa maslahi ya jamii.
Amesema
kupitia mfano uliooneshwa na Puma Energy Tanzania wa kuwakutanisha
wadau wake kila mwaka ili kuzungumzia mafanikio na changamoto
zilizopatikana, iwe ni chachu kwa kampuni nyingine kuiga mfano huo
ambao unasaidia kukuza sekta ya Nishati nchini.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania,
Bi. Fatuma Abdallah ameishukuru Serikali kwa hatua mbalimbali za
kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na kuahidi kuendelea
kuunga mkono juhudi hizo kwa kuwafikishia wananchi bidhaa ya Puma Gas
kupitia kwa Mawakala na Wadau waliopo maeneo mbalimbali.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Kamishna wa Petroli na Gesi, Godluck Shirima.
No comments