Serikali ya Rais Samia yatoa Trilioni 6 kwenye miradi ya maendeleo
Na Mwandishi Wetu
Ofisi
ya Rais imeendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kusogeza
huduma bora karibu na wananchi na kuwapunguzia adha walizokua wanazipata
hapo awali katika eneo la Afyamsingi, Elimumsingi, uboreshaji wa
miundombinu, ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na
utawala bora.
Katika
kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani Machi 19, 2021
hadi Februari 2024 Ofisi ya Rais -TAMISEMI imepokea zaidi ya Shilingi
Trilioni 6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Taarifa
hii ni kwa mujibu wa muhtasari wa mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali
ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia tangu aingie madarakani
uliotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI).
#KAZI INAONGEA
No comments