Rais Samia aboresha Afya msingi Mijini na Vijijini
#KAZI INAONGEA
Serikali
ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
imeendelea kufanya maboresho katika eneo la ujenzi wa miundombinu ya
kutolea huduma za Afya ya Msingi na ununuzi wa Vifaa Tiba.
Katika
kipindi cha uongozi wake kiasi cha Shilingi bilioni 916.6 kimetolewa
kwa ajili ya kuboresha eneo hilo, ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni
624,888 zilitolewa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati
wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya ya Msingi, Shilingi bilioni
287.5 kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa na Vifaa Tiba na Shilingi bilioni
4.21 zilitolewa kwa ajili ya kuendesha mafunzo mbalimbali kwa watoa
huduma ikiwemo mafunzo kwa wataalam wa kutoa huduma ya ganzi na usingizi
na mafunzo kwa wataalam wanaotoa huduma kwa wagonjwa mahututi na
wagonjwa wa dharura.
Hatua
hii ni mwenedelezo wa dhamira ya Rais Samia ya kumletea maendeleo
Mtanzania popote pale alipo, ambapo mara zote amekuwa akiamini kuwa
mwananchi mwenye afya njema ana uwezo wa kuzalisha.
Hii
ni kwa mujibu wa muhtasari wa mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya
Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia tangu aingie madarakani
uliotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI).
No comments