Breaking News

RAIS MWINYI AFUNGUA MAONESHO YA SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO 2024, asema Mikakati ya Rais Samia imeongeza Idadi ya Watalii


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DKt. Hussein Ali Mwinyi akifungua Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili (8th edition of the swahili international tourism expo – S!TE 2024) katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam.


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza wakati wa ufunguzi wa Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili (8th edition of the swahili international tourism expo – S!TE 2024) katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam.



Habari mbalimbali katika picha wakati wa ufunguzi wa Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili (8th edition of the swahili international tourism expo – S!TE 2024) katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam.

Na Mwanndishi Wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DKt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kutokana na Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan  idadi ya watalii wa kimataifa wanaotembelea nchini imekua kwa kasi sambamba na ongezeko la mapato yatokanayo na sSekta ya utalii. 

Amebainisha hayo leo Oktoba 11, 2024 wakati akifungua Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili (8th edition of the swahili international tourism expo – S!TE 2024) katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam ambalo limewakutanisha wanunuzi wa bidhaa za utalii, Waoneshaji, Wawekezaji na wadau mbalimbali wa utalii wa ndani na nje ya Tanzania.

Rais Mwinyi ametumia fursa hiyo kuipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa jitihada kubwa za kuongeza mapato yatokanayo na Sekta ya utalii katika kipindi kifupi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Kutokana na juhudi hizo za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, idadi ya watalii wa kimataifa wanaotembelea Nchi yetu imekua kwa kasi sambamba na ongezeko la mapato yatokanayo na sekta ya utalii. Mathalan, hadi kufikia mwezi Agosti, 2024 Tanzania imepokea jumla ya watalii wa kimataifa 2,026,378 ikiwa ni takwimu za juu kabisa kuwahi kufikiwa katika historia ya Nchi yetu. Pia, mapato yatokanayo na sekta ya utalii yamefikia Dola za Marekani bilioni 3.5”. amesema Dkt. Mwinyi na kuongeza,

"Sekta ya Utalii imeendelea kuwa nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania, huku ikichangia asilimia 17.2 ya Pato Ghafi la Taifa, asilimia 25 ya mauzo ya nje na kuzalisha ajira zaidi ya milioni 1.5 ikiwa ni ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kupitia mnyororo wake wa thamani,".

Ameeleza  kuwa mafanikio hayo yamewezesha nchi yetu kutambuliwa kimataifa na kupata tuzo mbalimbali ambapo taarifa iliyotolewa mwezi Septemba, 2024 na Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism – World Tourism Barometer) ambapo inaonesha kuwa, Tanzania imeshika nafasi ya 6 Duniani na ya kwanza Barani Afrika kwa kuwa na ongezeko kubwa la watalii.  

Ametaja miongoni mwa tuzo hizo kuwa ni zile zilizotolewa mwaka 2023 na World Travel Awards (WTA) ambao wameitambua Bodi ya Utalii Tanzania kama Africa’s Leading Tourist Board, Kisiwa cha Thanda Shunghumbili, Mafia kama World Leading Exclusive Private Island, Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kama Africa’s Leading Tourist Attraction.


No comments