Breaking News

“UANDIKISHAJI WA WAPIGAKURA KWA SIKU 9 WAFIKIA ASILIMIA 81” MCHENGERWA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa

Juma ya Wapiga kura 26,769,995 sawa na asilimia 81 ya kuandikisha wapigakura 32,987,579 wameandikishwa kwenye daftari la wapigakura wa Serikali za Mitaa hadi kufikia tarehe 19/10/2024 ambayo ni siku ya 9 ya uandikishaji wa wapiga kura.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokua akitoa taarifa ya mwenendo wa uandikishaji wa wapigakura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 tarehe 20.10.2024 kwenye Halmashauri ya Rufiji mkoani Pwani.

Amesema hali ya uandikishaji wa wapiga kwa siku tisa ni nzuri na jumla ya wapiga kura 26,769,995 wamejiandikisha kupiga kura sawa na asilimia 81.15 ya lengo la kuandikisha watu 32,987,579 kwa siku zote 10.

“Jumla ya uandikishaji kwa wanaume ni 13,033,988 sawa na asilimia 48.69 ya watu wote waliojiandikisha kwa tarehe 11-19 Oktoba, 2024 na wanawake ni 13,736,007sawa na asilimia 51.31 ya watu wote waliojiandikisha”
 
Amesema kwa ujumla, mwenendo huu ni mzuri na unaridhisha, na kama tutamalizia hivi kwa siku ya leo, uwezekano wa kufikia malengo ya uandikishaji ni mkubwa sana.

Alibainisha mwenendo wa uandikishaji kuanzia siku ya 5 hadi ya 9 kuwa kumekuwa na kuongezeka kwa idadi ya Watanzania waliojitokeza kujiandikisha kuanzia Siku ya 5 ya tarehe 16 Oktoba, 2024 ambapo waliandikishwa jumla ya wapiga kura 2,460,664 sawa na asilimia 7.46 ya lengo la siku la kuandikisha asilimia 10;

Aidha katika Siku ya 6 tarehe 16 Oktoba, 2024 waliandikishwa jumla ya wapiga
kura 2,472,605 sawa na asilimia 7.50 ya lengo la siku la kuandikisha asilimia 10  na Siku ya 7 tarehe 17 Oktoba, 2024 waliandikishwa jumla ya wapiga kura 2,971,219 sawa na asilimia 9.01 ya lengo la sikula kuandikisha asilimia 10.

Pia kwa Siku ya 8 tarehe 18 Oktoba, 2024 waliandikishwa jumla ya wapiga kura 3,409,211 sawa na asilimia 10.33 ya lengo la siku la kuandikisha asilimia 10 na Siku ya 9 tarehe 19 Oktoba 2024 waliandikishwa jumla ya wapiga kura  3,813,999 sawa na asilimia 11.6 ya lengo la siku la kuandikisha asilimia 10.
 
Mhe. Mchengerwa ametaja Mikoa mitano yenye asilimia kubwa ya uandikishaji hadi kufikia tarehe 18 Oktoba, 2024 kuwa ni Mkoa wa  Tanga umefikia asilimia 101.13% ulifuatiwa na Pwani asilimia 98.74% kisha 
Mwanza umefikia asilimia 94.09%, Dar Es Salaam umefikia asilimia 86.66%  na Dodoma umefikia asilimia 80.63% ya malengo.
 
Kufuatia mwenendo huu mzuri wa uandikishaji, nichukue fursa hii kuwashukuru na kuwapongeza Watanzania wote waliojitokeza kujiandikisha hadi kufikia tarehe 19 Oktoba 2024 kwa kuwa tayari wamejiwekea mazingira yanayokubalika kisheria ya kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa wanaowataka ifikapo tarehe 27 Oktoba 2024 siku ya kupiga kura’ alisema

Mwisho Mhe Mchengerwa alisisitiza kuwa  hakuna siku zitakazoongezwa kwa ajili ya uandikishaji  wa wapigakura wa Serikali za Mitaa tarehe 20.10.2024 ifikapo saa kumi na mbili jioni ndio itakua mwisho wa zoezi hili la uandikishaji.

No comments