Breaking News

Mama Samia afanikisha huduma muhimu Vituo 132 Vya Afya

 #KAZI INAONGEA

Ikumbukwe kuwa tangu nchi hii inapata uhuru wake mwaka 1961, vituo vya kutolea huduma za Afya yaani (Zahanati, vituo vya Afya  pamoja na hospitali za Wilaya) havijawahi kuwa na majengo ya dharura (EMD), majengo ya wagonjwa mahututu (ICU) pamoja mitambo ya kuzalisha hewa tiba ya Oksijeni.

Lakini katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi thabiti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweza kupambana na kufanikisha kupatikana kwa huduma hizo muhimu katika vituo 132 vya Afya hapa nchini na lengo likiwa ni kuokoa maisha ya mwanadamu.

Ni wazi kuwa, wengi wetu tulidhani sio viwango vya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kuweza kupatikana huduma hizi.

Juhudi hizi za Rais Samia, zinapaswa kupongezwa na kuungwa mkono kutokana na kuonyesha moyo na jitihada katika kuokoa maisha ya Watanzania. 

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, asilimia 75% ya Watanzania wote wanatibiwa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya nchini lakini pia asilimia 80 ya wajawazito wote wanajifunguliwa kwenye vituo hivyo.

Hadi kufikia Machi 2024, Wizara ya Afya imetekeleza kwa mafanikio majukumu yake, 
ikijikita katika maeneo makuu mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya 
kutolea huduma za Afya nchini, hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya, upatikanaji wa 
huduma za kibingwa bobezi nchini.

Mbali za huduma hizo muhimu, lakini pia imefabikisha kupatikana kwa huduma za uchunguzi wa mionzi, huduma 
za Afya ya uzazi na mtoto, magonjwa ya 
mlipuko, ajira kwa watumishi, udahili wa 
wanafunzi, upatikanaji wa watoa huduma 
ngazi ya jamii (CHWs) na Sheria ya Bima ya 
Afya kwa wote. 

Hii inaonyesha wazi kuwa, endapo Mama Samia asingesimamia vyema Sekta ya Afya na kuboresha vituo vya afya kwa kuongeza miundombinu kwa kiwango hiki alichofanya, hali ya watanzania kwa upande wa Afya ingekuwa mbaya.

 # KAZI INAONGEA

No comments