KAWAIDA AMJIBU LEMA, HIZI HAPA SABABU ZILIZOWAFANYA VIONGOZI WA CHADEMA KUTIMKIA CCM
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida akihutubia wananchi wa Jimbo la Ngara Mkoani Kagera Oktoba 17, 2024. Na, Mwandishi wetu - Fichuzi Blog. |
Kufuatia Kauli za kiongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godless Lema zilizozua taharuki katika mitandao ya kijamii kuwakashfu baadhi ya viongozi na wasimamizi wa uandikishaji daftari la mkazi akilalamikia kutokufuata taratibu rasmi Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida ameonyesha kustaajabishwa na jambo hilo.
Hayo yamejiri leo Oktoba 16, 2024 Wilayani Ngara Mkoani Kagera wakati alipokuwa kwenye ziara ya kawaida ya kukijenga Chama ambapo pamoja na mambo mengine ametolea ufafanuzi wa mada hiyo na kwamba haina uhalisia bali analenga kuvuruga uchaguzi kwa kupotosha umma.
"Leo Asubuhi wakati naangalia mitandaobya kijamii nikamuona kiongozi mmoja wa upinzani Godless Lema akilalamika na kuaminisha umma eti Kuna mambo ya ovyo yanafanyika, kuwa wakurugenzi wa uchaguzi na mawakala wanaosajili watubkwenye madaftari ya makazi kwamba wanawasajili wanafunzi wa shule katika lile Daftari". Amesema Kawaida
“Tunalaani kitendo hichi, wanataka tuwapore watu haki zao za msingi?, tunawataka waendelee kusajili muhimu wawe wametimiza umri wa kupiga kura hata kama bado anasoma, wangetumia muda mwingi wa malalamiko kuwahamasisha watu waende kujiandikisha na waweze kupigiwa kura” Kawaida.
Ikumbukwe kuwa kauli hiyo imekuja mara baada ya Godbless Lema kudai kuwa baadhi ya vituo vya uandikishaji havifanyi kazi kwa uadilifu na kwamba baadhi ya maafisa wa uandikishaji wanakwepa taratibu rasmi hivyo haridhishwi na mwenendo wa zoezi hilo linaloendelea Nchini.
Aidha katika Mkutano huo Kawaida akiambatana na viongozi wengine wamepokea wanachama wapya waliokuwa viongozi watatu kutoka Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA na kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM huku chanzo wakieleza ni kuridhishwa na maendeleo wanayoyapata nchini yatokanayo na Utekelezaji wa Ilani ya Chama tawala CCM.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida amempongeza Mbunge wa jimbo hilo kwa jitihada anazozifanya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kuanzia ngazi ya jamii ikiwa ni pamoja na kuwainua kiuchumi.
|
Sehemu ya wananchi walioshiriki katika Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera. |
Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro akihutubia mamia ya wananchi walioshiriki kwenye Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera. |
Wananchi wakifurahia jambo katika Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera. |
Picha za Matukio Mbalimbali wakati wa Mkutano wa Mwenyekiti wa umoja wa vijana Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa Kawaida Alli Kawaida Oktoba 17, 2024 Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/hzJ2Xgf
No comments