Breaking News

WAKALA WA VIPIMO YAJIVUNIA ONGEZEKO LA VIPIMO, yaendelea kuchangia katika Mfuko Mkuu wa Serikali

                                Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Alban Kihulla

                               Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile 
              Sabato Kosuri Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Mawasiliano

NA MWANDISHI WETU

WAKALA wa Vipimo (WMA) inajivunia kuongezeka kwa idadi ya vipimo vinavyohakikiwa ikiwa ni moja ya mafanikio yake.

Hayo yamebainishwa jana na Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA Alban Kihulla akizungumza katika kikao cha Wahariri wa Vyombo mbalimbali na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.

Akiainisha namna idadi ya vipimo vinavyohakikiwa ilivyoengozeka alisema kwa mwaka wa fedha 2018/2019 idadi ya vipimo ilikuwa 837,306, kwa mwaka wa fedha 2019/2020 idadi ya vipimo ilikuwa 841,603, kwa mwaka 2020/2021 idadi ya vipimo ilikuwa 975,203, huku kwa mwaka wa fedha 2021/2022 idadi ya vipimo ilikuwa 986,342 na mwaka wa fedha 2022/2023 idadi ya vipimo ilikuwa 949,565.

Kwamba mafanikio mengine ni kuendelea kuchangia katika mfuko mkuu wa Serikali ambapo kwa mwaka 2 0 1 8 / 2 0 1 9  mchango ni 4.0,  mwaka 2 0 1 9 / 2 0 2 0  mchango ni 5.3, mwaka 2 0 2 0 / 2 0 2 1 mchango ni 6.4, mwaka 2 0 2 1 / 2 0 22 mchango ni 4.2 na mwaka 2 0 2 2 / 2 0 2 3 mchano ni 4.3.

Kihulla aliongeza mafanikio mengine kuwa ni kuendelea na Ununuzi wa vifaa vya Kitaalam.

Hata hivyo Pamoja na mafanikio hayo alibainisha changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni Pamoja na ongezeko la uelewa kuhusiana na matakwa ya Sheria ya Vipimo, Maboresho ya Mazingira ya ufanyaji Biashara nchini Tanzania, Mabadiliko ya Teknolojia, Uwepo wa watumishi wachache wa ajira kudumu ambapo waliopo ni 267, hiaji ni 581, hivyo pungufu ni 314 na wenye mkataba ni 153.

Kuhusu maono ya mbele ya WMA Kihulla alisema ni kuingia kwenye maeneo mapya ya uhakiki wa Vipimo, kuendelea kutoa Elimu kuhusiana na Matakwa ya Sheria ya Vipimo, kuendelea kuboresha mifumo ya utendaji kazi na kuendelea kujenga uwezo (Mafunzo na ununuzi wa vifaa).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile aliipongeza WMA kwa utakelezaji wa majukumu yake kwa kuhakikisha wananchi wanapata vipimo sahihi, kwa huduma na bidhaa wanazonunua.

Aliongeza kwa kuishauri WMA kutengea bajeti ya shilingi bilioni moja kwa vyombo vya Habari ili kusaidia kutangaza majukumu yao na kuwafikishia wananchi taarifa mbalimbalimbali zinazowahusu.

Hata hivyo aliiomba kuhakikisha inatizama zaidi kwenye vifaa vya ujenzi ili wananchi waweze kupata bidhaa au huduma stahiki zinazoendana na thamani ya fedha zao kwa sababu wananchi wamekuwa wakilalamika kupata huduma au bidhaa hizo zikiwa chini ya kipimo tegemewa. Hivyo aliwasisitiza kuongeza ufuatiliaji juu ya jambo hilo.

Miongoni mwa majukumu ya Wakala ni Pamoja na kuhifadhi vipimo vyenye usahihi wa ngazi ya kati (secondary Standards), kuilinda jamii kuepukana na madhara yatokanayo na matokeo ya upimaji usio sahihi katika Biashara.

Mengine ni kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika kwenye Sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira,  kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusiana na vipimo kwa Serikali, Mashirika, Taasisi na wadau Wengine na kusimamia matumizi sahihi ya vipimo kwa njia ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara (Scheduled and Surprised Inspections).

No comments