TEMESA kufanya mageuzi makubwa ya huduma za karakana, vivuko,ukodishaji mitambo kwa ubia sekta ya umma,binafsi
Utekelezaji
wa miradi ya taasisi za umma kwa ubia
baina ya za umma na binafsi umeibainika kuwa ni njia sahihi katika uanzishwaji na
utekelezaji wa miradi ya taasisi za umma. Hivi karibuni, idadi ya taasisi za umma zinanzovutiwa kutekeleza miradi
yake ya maendeleo kwa njia ya Ubia kati ya sekta
ya umma na binafsi, imekuwa ikiongezeka kila
kukicha.
Wakala
wa Ufundi na Umeme (TEMESA), umetangaza
fursa adhimu kwa wawekezaji binafsi ndani
na nje
ya nchi kuonyesha nia ya kuwekeza, kuboresha na kuendesha karakana zake kupitia
njia ya Ubia.
Kama
invyofahamika na kwa mujibu wa sheria iliyoianzisha TEMESA, kuwa jukuimu na wajibu wake ni kufanya matengenezo ya
magari, pikipiki na mitambo ya Serikali katika karakana ambazo zipo kila mkoa.
Vile vile, inafanya shughuli za uendeshaji wa vivuko vya Serikali na kukodisha
mitambo kwa wadau wanaofanya shughuli za ujenzi wa miundombinu.
TEMESA
inasimamia mtandao wa karakana thelathini (30) katika mikoa 26 nchini, ambazo
kwa wastani zinahudumia magari takriban 29,263 kwa mwaka. Pia, TEMESA inakarabati
na kuhudumia magari ya serikali yapatayo 9,183, pikipiki 12,778 na vifaa au
mitambo 433. Aidha, TEMESA inaendesha vivuko 32 katika mikoa 12
na maeneo ya kuvuka 22 kote nchini.
Takriban
abiria 79,863 na magari 3,696 hupita katika vivuko hivi kila siku. Serikali
inajenga vivuko vipya nane ambapo vitano vitafanya kazi katika Ziwa Victoria na
vitatu katika Bahari ya Hindi. Fursa nyingine za uwekezaji zilizopo kwenye
vivuko hivi ni pamoja na ardhi, majengo na miundombinu muhimu kama sehemu za
kusubiria abiria, migahawa, ofisi na mifumo mbalimbali. Pia, Wakala unamiliki
mitambo ya aina mbalimbali 41 kwa ajili ya kukodisha kwa wateja kwenye sekta za
umma na binafsi.
Katika
nia za kuimarisha ufanisi na ubora, TEMESA imedhamiria kuendesha karakana zake
kumi na tatu (13) kwa njia ya ubia. Karakana hizi ziko katika mikoa ya Katavi,
Rukwa, Shinyanga, Kagera, Singida, Iringa, na Mara.
Mikoa mingine ni pamoja na Manyara,
Pwani, Lindi, Ruvuma, Njombe, na Simiyu. Vile vile, Wakala unakusudia kuendesha
huduma zote za vivuko nchini kupitia kwa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi
(PPP). Mwekezaji ataruhusiwa kukodisha huduma za kivuko chote, kuunda kampuni
ya ubia na TEMESA, au kuendesha vivuko vyake sambamba na vivuko vya TEMESA.
Aidha, Wakala unakusudia kumshirikisha mwekezaji binafsi katika kutoa huduma za
ukodishaji wa vifaa kwa njia ya ubia kati ya TEMESA na mwekezaji.
Hatua
hii ya kimapinduzi ya TEMESA inaungwa mkono kikamilifu na mfumo wa kisheria wa
utekelezaji wa miradi kwa njia ya ubia, ambapo Kanuni za 36 (b) & (d) za
Kanuni za Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi za mwaka 2020 kama
zilivyorekebishwa mwaka 2023, zinairuhusu TEMESA kuwaalika wawekezaji katika
utekelezaji wa miradi yake kwa njia ya ubia.
Mpango
wa TEMESA wa kuboresha karakana zake, vivuko na kutoa huduma ya ukodishaji
mitambo kwa njia ya Ubia unatoa matumaini ya kukidhi mahitaji makubwa ya huduma
hizi yaliyopo kwenye soko. Ushirikishwaji wa wawekezaji utaleta manufaa mengi
ikiwepo kuvutia teknolojia za kisasa, kuchochea ufanisi wa uendeshaji wa
karakana na vivuko pamoja na kuboresha ubora wa huduma za Wakala kwa ujumla
wake.
Kituo
cha Ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, chini ya uongozi mahiri wa
Mkurugenzi Mtendaji wake, Bw. David Kafulila, kimekuwa ni kiungo muhimu katika
kusaidia taasisi za Umma kubuni miradi inayofaa kutekelezwa kwa njia ya ubia.
Tangu
Kituo cha Ubia kilipoanzishwa rasmi mapema mwaka huu, nchi imeshuhudia mabadiliko
makubwa kwenye uratibu wa miradi kwa njia ya Ubia. Mageuzi makubwa yatazidi
kutokea katika miradi ya Ubia baada tu ya Kituo kufikia adhma yake ya kutoa
huduma zote za ubia ndani ya Kituo (one-stop centre).
No comments