Breaking News

Naibu Waziri Chumi na Balozi wa Japan wakutana Jijini Dodoma

 Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi amekutana na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yasushi Misawa aliyemtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma. 

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Japan kwa manufaa ya pande zote.

 



Mhe. Chumi aliishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kupitia sekta mbalimbali na hivyo kuunga  mkono jitihada za Serikali katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

 

Mhe. Chumi pia amemhakikishia Mhe. Balozi Misawa kuwa Tanzania inajali na kuthamini uhusiano wake na Japan na kumuahidi kuwa  Mamlaka ya Biashara Nje (Tantrade) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Japan wanaendelea na maandalizi ya kushiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara yatakayofanyika Osaka nchini Japan mwaka 2025.

 

Naye Balozi wa Japan Mhe. Misawa ameelezea utayari wa nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa manufaa ya pande zote mbili.

 

Pia ameshukuru Ushirikiano anaoupata kutoka Serikali ya Tanzania na hivyo kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

 

Tanzania na Japan zinashirikiana kupitia sekta za biashara na uwekezaji, miundombinu, afya na masuala ya kodi


No comments