Breaking News

WIZARA YA ELIMU YAKUTANA NA WADAU KUPOKEA MAONI KUBORESHA MPANGO WA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Charles akizungumza katika Mkutano wa kutoa maoni kuboresha mpango wa maendeleo ya sekta ya elimu 2021/2022- 2025/2026, leo Agosti 19, 2024 Jijini Dar es Salaam.

********************

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekutana na wadau ili kupokea maoni ya Rasimu ya Mapitio ya Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu 2021/22 - 2025/26 yatakayowezesha kufikia malengo, shabaha na kutekeleza mikakati ya kuendeleza Sekta ya Elimu nchini.

Akizungumza Agosti 19, 2024 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa mkutano wa wadau hao, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Charles amesema kuwa rasimu ya mpango huo imeandaliwa na kikosi kazi maalum, hivyo mkutano huo unalenga kupata maoni kutoka kwa wadau ili kuiboresha rasimu hiyo na iweze kutekelezwa kwa ufanisi.

Dkt. Charles amesema kuwa ni muhimu kwa wadau hao kutoa maoni kwa kuzingatia mabadiliko katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo, Mitalaa na pia kuzingatia taarifa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Nae Mwenyekiti wa kundi la wadau wa Maendeleo na Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO Faith Shayo amesema kuwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu ni muhimu kwa kuwa unatoa dira katika maeneo na nyaja mbalimbali ambazo ni vipaumbele vya serikali ambavyo vinawezesha wadau kushiriki katika hatua za maendeleo.

Ameongeza kuwa amefurahishwa kuona Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilivyoweza kushirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo wanafunzi wa Msingi na Sekondari, Vyuo vya Elimu ya Juu na Kati katika mkutano huo.

"Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu ni wetu sote na nina furaha kuona pia umekuwa shirikishi hivyo unawapa wadau mbalimbali nafasi kuuangalia, kuuelewa na kutoa maoni ili utuongoze kwa miaka mitano tukiwa na uelewa na bia moja," amesisitiza Shayo
Mkurugenzi Msaidizi anaesimamia elimu awali na msingi OR- TAMISEMI Mwl. Suzan Nyarubamba akimwakilisha Katibu Mkuu OR- TAMISEMI, akizungumza katika Mkutano wa kutoa maoni kuboresha mpango wa maendeleo ya sekta ya elimu 2021/2022- 2025/2026, leo Agosti 19, 2024 Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa kundi la wadau wa Maendeleo na Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO Faith Shayo akizungumza katika Mkutano wa kutoa maoni kuboresha mpango wa maendeleo ya sekta ya elimu 2021/2022- 2025/2026, leo Agosti 19, 2024 Jijini Dar es Salaam
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akizungumza katika Mkutano wa kutoa maoni kuboresha mpango wa maendeleo ya sekta ya elimu 2021/2022- 2025/2026, leo Agosti 19, 2024 Jijini Dar es Salaam
Wadau mbambali wa sekta ya elimu wakiwa katika Mkutano wa kutoa maoni kuboresha mpango wa maendeleo ya sekta ya elimu 2021/2022- 2025/2026


from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/z4UIBpl

No comments