WAFANYABIASHARA TANGA WATOA USHAURI KWA BENKI YA NMB WALIOCHUKUA MIKOPO NA KUSHINDWA KUIREJESHA
Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga (JWT) Ismail Masoud akizungumza wakati wa mkutano huo
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus akizungumza wakati wa mkutano huo |
Na Oscar Assenga, TANGA.
JUMUIYA ya wafanyabiashara Mkoa wa Tanga JWT imeiomba Benki ya NMB nchini kuweka utaratibu nzuri wa kudai madeni yao kwa wafanyabiashara waliochukua mikopo kwa kuunda kamati kila wilaya ambazo zitaratibu na kufuatilia walioshindwa kuilipa waone njia sahihi ya ya kulipwa badala ya kufikiria kuwauzia nyumba zao na mali ili kufidia mikopo hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Masoud Ismail wakati wa mkutano wa Business Club 2024 uliofanyika Jijini Tanga ambapo alisema wanataka wafanyabiashara wasiuziwe nyumba zao na mali wanazomiliki bali ziundwe kamati za madeni kila wilaya zitakayowezesha upatikanaji wa fedha zinazodaiwa.
Alisema kwamba kamati hizo zihusishe wafanyabiashara wenyewe kwamba mfanyabiashara amekutana na changamoto badala ya kwenda kuuza nyumba yake deni lipelekewe kwenye kamati ya wafanyabiashara wenyewe kwamba anadaiwa na anatakiwa kwenda kuuziwa nyumba yake wafanyaje na itakuwa ni benki ya kwanza kuwashirikisha wafanyabiashara wenyewe kusaidia kulipa madeni badala ya kuuza nyumba.
“NMB chukueni Sera hii na mkiifanya mtafanikiwa nchini nzima kwamba kila wilaya kuwa na kamati ya Madeni ikihusisha wafanyabiashara na unakuta mtu nyumba ikienda kuuzwa anadaiwa milioni 3 hivyo wakikutana wanaweza kuchangishana na kuweza kumaliza deni hilo”Alisema
Aidha alisema kwamba biashara zimekuwa na changamoto nyingi hasa ushindani umekwa juu wafanyabiashara kupitia ushindani wa mifumo ya biashara unawaumiza na bahati mbaya wanashindana na watu wasiolipa kodi kwenye biashara ambazo wanazifanya wao.
“Lakini wengine hawalipi kodi hilo ni tatizo linawaumiza wafanyabiashara hivyo NMB lazima tubadilishe sera asilimia 60 ya wafanyabiashara nchini ni wamachinga hawalipi kodi asilimia 40 ni wafanyabiashara wanaolipa kodi na kuchukua mikopo kwao kuna namna mbili wanatakiwa kufanya biashara walipe kodi na wanatakiwa kufanya biashara kurudisha mikopo hivyo mifumo ya mabenki lazima ibadilike kulingana na hali biashara ilivyo”Alisema
Aidha alisema kwamba wasipobadilisha sera hali ya biashara itaendelea kuwa ngumu na wafanyabiashara hawataki akaunti zao zikamatwe na wanaaza kurudi nyuma kwenye mfumo wa Tanzania kutunza fedha kwenye vitanda kwa sababu akaunti zao zinakamatwa na TRA wafanyaboashara hawataki.
Alisema kwamba benki akaunti ni siri ya mtu na benki na wanataka mfumo wa kutumia fedha taslimu uachwe watumie swap sasa benki na JWT na TRA wanashindwa kutumia njia zipi za watu wanadaiwa wafanywaje walipe mpaka wanakwenda kuingilia akauti za watu wanalalami fedha zao.
“Niwaambie kwamba benki ndio zinafanya kazi sana kuliko mitandao lakini Tanzania mitandao ndio inafanya kazi zaidi kuliko benki na mifumo ya fedha Tanzania inazunguka sana kwenye mifumo ya mitandao kuliko benki inabidi tushirikina na sisi Jumuya za wafanyabiashara tuone namna ya kufanya mifumo ya fedha ipitie kwenye mabeki
Awali akizungumza Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Baraka Ladislaus alisema kwamba leo la kuanzishwa kwa NMB Business ni kuwafanya wateja wao wawe karibu na wao lakini kupitia huko wanapat fursa ya kusikia changamotoo mbalimblai za wateja wao na hivyo kuwasaidia kufanya maboresho katika huduma ambazo wamekuwa wakizitoa.
“Ni matumaini yangu baada ya kusikia mada mbalimbali zitakazotolewa nanyi watapata fursa ya kuwapa maeneo yenu ili waendelea kuyachukua na kuyachakata na kuzipatia ufumbuzi na kujenga NMB na wateja walio imara”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba benki hiyo itaendelea kuboresha huduma zake katika maeneo mbalimbali na sasa wameendelea kuwafikia wateja wadogo wadogo wa kule chini na akaunti za NMB zimeboresha.
“Maboresho makubwa ni kiu ya Benki ya NMB kuendelea kuwa chaguo lako ukitaka kuchagua benki NMB iendelea kubaki kuleta huduma za kibunifu zitakazoleta matokeo chanya kwa wateja wetu”Alisema
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/2ohdlKj
No comments