Breaking News

TANESCO,REA ZASHAURIWA KUNUNUA TRANSFOMA TANALEC, GENERAL TYRE KUFUFULIWA

 

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiangalia Transfoma zinazotengenezwa na Kiwanda cha TANALEC Limited wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024.

 

......

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) ametoa rai kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuongeza kasi ya ununuzi wa transfoma zinazozalishwa na Kiwanda cha Tanelec kwa kuwa Taasisi hizo ni wamiliki wa sehemu ya hisa za kiwanda hicho ili kukiwezesha kiendelee kukua na kuongeza ajira nchini.

Dkt Jafo ameyasema hayo Agosti 24, 2024, Mkoani Arusha, alipotembelea viwanda, kuongea na Wafanyabiara pamoja na Maafisa Biashara wa Mkoa huo kwa lengo la kujionea shughjuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto na kuona njia bora ya kuzitatua kwa kushirikiana na Taasisi nyingine husika ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Aidha, Dkt Jafo amelielekeza Shirika la Taifa la Maendeleo NDC kuhakikisha linapata mwekezaji makini kwa ajili ya Kiwanda cha Matairi cha General Tyre East Africa (GTEA) Limited ili kifufuliwe na kuanza uzalishaji wa matairi lengo la kuongeza ajira na patonla taifa kwa ujumla

Katika hatua nyingine akiongea na Wafanyabiashara, Wamiliki wa Viwanda na Maafisa Biashara wa Mkoa wa Arusha, Waziri Jafo ametoa rai kwa Watanzania kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa sekta ya viwanda na biashara inasonga mbele kwa kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuboresha mazingira ya biashara ikiwemo miundombinu ya maji, barabara, reli, umeme na matlrekebisho mbalinbali ya Sera Sheria na Kanuni.

Aidha, Dkt Jafo amebainisha kuwa akiwa Mkoani humo ametembelea Kiwanda cha Maziwa cha Tanzania Dairies Limited (TDL), Kiwanda cha Kilimanjaro Textile Mills Limited (Kilitex), Kiwanda cha General Tyre East Africa (GTEA) Limited, Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited, Kiwanda cha Kutengeneza Transfoma cha TANELEC Limited, Kiwanda cha nguo cha Sunflag na Kiwanda Moonlight Tanzania Limited

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda ameaidi kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na TAMISEMI ili kuhakikisha changamoto zote za wafanyabiashara zinatatuliwa kwa hatua ili kuhakikisha viwanda vyote mkoani humo vinafanya kazi na Mkoa wa Arusha unakiwa Mkoa wa Mfano katika kuendeleza viwanda na kukiza biashara.

Naye Mkurugenzi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe amesema NDC imepokea maelekezo yote na itayafanyia kazi ilinkuhakikisha kiwa kiwanda cha General tiyre kinafuguka na kufanya kazi kwa ufanisi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) na ujumbe wake akitembelea Kiwanda cha Maziwa cha Tanzania Dairies Limited (TDL) kilichopo Unga Limited wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki hakifanyi kazi tangu kilipobinafsishwa 1998.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) na ujumbe wake akitembelea Kiwanda cha Kilimanjaro Textile Mills Limited (Kilitex), kilichopo Themi Hill wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki kilibinafsishwa na hakifanyi kazi.

aziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) na ujumbe wake akitembelea Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Limited kilichopo Njiro wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki hakifanyi kazI.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) na ujumbe wake akitembelea na kuongea na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Transfoma cha TANALEC Limited Bw. Zahir Saleh wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki kinafanya kazi na kinauwezo wa kutengeneza Transiformer 14,000 kwa mwaka na zinauzwa ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiangalia Transfoma zinazotengenezwa na Kiwanda cha TANALEC Limited wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akizungumza na Wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo cha Sunflag wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki kinafanya kazi na kimeajiri takribani wafanyakazi 2800 na kinauza bidhaa zake ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akiongea na Wafanyakazi wa Kiwanda Moonlight Tanzania Limited wakati wa ziara yake Mkoa wa Arusha Agosti 24, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini. Kiwanda hiki kinafanya kazi na kinauza bidhaa zake ndani na nje ya nchi



from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/cV25myH

No comments