Breaking News

Rais Samia aombwa kuingilia kati mgogoro wa ardhi Salasala Dar Es Salaam,wananchi wahofia usalama wao.


Wananchi wakionyesha nyaraka mbalimbali zinazohusiana na mgogoro huo

NA MWANDISHI WETU

WAKAZI wa Mtaa wa Sala Sala, Zoni ya Upendo Kata ya Wazo, mkoani Dar es Salaan wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi kuingilia kati mgogoro wa ardhi baina yao na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wakazi hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 1500, muhusika mkuu wa katika mgogoro huo Gerry Kakiziba ambaye pia ni Mwanahisa wa kampuni ya Global Minging Company Limited ilichokuwa kikijishughulisha na uchimbaji wa kokoto,mawe na kifusi alisema mgogoro huo unatokana na Halmashauri kutaka kuwarasimishia maeneo yao kwa kuwauzia kwa shilingi 6614 kwa kila 'square' mita moja jambo ambalo hawakubaliani nalo.

Kwamba kiasi hicho ni kikumba ambacho kinafanya kuwa jumla ya shilimbi milioni 6 kwa kiwanja kimoja, tofauti na awali ambapo aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willium Lukuvu aliagiza warasimishiwa maeneo yako kwa shilingi laki moja na nusu (150,000) jambo ambali Halmashauri wanalikataa wakidai kuwa wanafanya hivyo kwa sababu eneo hilo ni mali yao.

Hata hivyo Kakiziba alikanusha kuwa eneo hilo sio la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwani ameishi katika ardhi hiyo tangu mwaka 1983 na kwamba Halmashauri iliibuka kudai eneo hilo ni mali yao baada ya lililokuwa Jiji la Dar es Salaam kuvunjwa na kila Halmashauri kutakiwa kuchukua mali zake, na hivypo Kinondoani kudai kuwa ni sehemu ya mali yao.

Alibainisha kuwa awali eneo hilo lenye ukubwa wa takribani eka 75 lilikuwa ni la machimbo ya mawe ya kokoto ambapo kila mwananchi alikuwa na eneo lake, lakini baada ya shughuli hiyo kwishi, waliamua kujenga nyumba na ndipo ilipangwa warasimishiwe kila mtu eneo lake kwa shilingi 250,000, lakini baadaye Waziri Lukuvi alibatilisha na kutaka kazi hiyo ifanyike kwa shilingi 150,000.

Pamoja na hilo, Waziri aliyepita wa Ardhi Silaa naye hivi karibuni kabla ya kupangiwa wizara nyimgine na Mhe Rais aliagiza warasimishiwe kwa shilingi 130,000, hata hivyo wakazi hao wanapendekeza warasimishiwe kwa shilingi 150,000 badala ya shilingi 6614 kwa kila square mita moja kama Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inavyotaka.

Kakiziba anadai kuwa nyumba ya pazia sababu ya wananchi wote kuingizwa kwenye utaratibu wa kurasimishiwa maeneo yao kwa shilingi 6614 kwa kila Square mita moja ni kwamba wanataka eneo lake la kampuni ya Global Mining Company Limited lenye ukubwa wa eka 18, huku akibainisha kuwa aliyeko nyuma ya chokochoko hizo ni Kamishna wa Ardhi Tanzania.

"Mwanzoni Halmashauri ilitaka wananchi warasimishiwe kwa shilingi 250,000, hata hivyo Waziri Lukuvi alibatilisha na kutaka iwe kwa shilingi 150,000 baada ya kuona wananchi wote ni wa hali ya chini, lengo kila mwananchi aweze kumudu gharama. Lakini pia Waziri Silaa naye alipunguza zaidi gharama hadi shilingi 130,000," alisema Kakiziba na kuongeza,

"Hata hivyo baada ya kuvunjwa kwa Jiji la Dar es Salaam na kila Manispaa kutakiwa kuchukua mali zake, eneo hili walilifanya ni sehemu ya mali yao na hivyo kuwataka wananchi kurasimishiwa maeneo yao kwa kulipia shilingi 6614 kwa kila 'square' mita moja, kitu ambacho hatukubaliani nacho. Sisi tunataka kwa shilingi 150,000,".

Alibainisha kuwa anasema hivyo kwa sababu anaushahidi wote juu ya jambo hilo na kwamba yupo tayari kuthibitisha hilo hata kwa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwani upo hata ushahidi kupitia nyaraka alizonazo zinazohusiana na mgogoro huo.

Vile vile alisema kutokana na mgogoro huo imefikia hatu ya kutishiwa bunduki na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambapo alifanyiwa tukio hilo hivi karibuni.

Aliongeza kuwa kama Global Mining Company Limited wapo tayari kutoa eneo la eka tatu kwa ajili ya ujenzi wa shule kwa ajili ya watogto wao, lakini wanachohitaji kwa sasa ni kupatiwa ardhi yao na hati miliki.

Kwa upande wake Amina Selemani mkazi wa eneo hilo, alimuomba Waziri wa Aridhi kuhakikisha gharama za urasimishaji zinapungua na kila mkazi alipie shilingie 150,000 kwa kiwanja.

"Tunataka tupewe viwanja vyetu na tusisumbuliwe tena, mara kwa mara wanatusumbua, wamekuwa wakija na kuweka alama za 'bomoa' kwenye nyumba zetu, hivyo tunaomba sana Rais na Waziri mtusaidie," amesema Selemani.

Naye Joseph Nyoni mkazi wa eneo hilo, alisema kama kweli eneo hilo ni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, wanapaswa kuthibitisha kwa kuonesha umiliki wao kwa hati na sio vinginevyo ambapo alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Dkt. Samia kuwasaidia kupata suluhu ya kudumu ya mgogoro huo.

Mpaka tunachapisha habari hii tumemtafuta wahusika wa Manispaa ya Kinondoni na Kamishna wa ardhi Dar es Salaam na Pwani ili kusikia upande wake kama serikali na watu wote waliotajwa katika katika hujma hizi zilizo tajwa na walamikaji hakuweza kutoa ushirikiano kwa mwandishi wetu.

No comments