Breaking News

Waziri Nape: Tuna wajibu wa kuilinda nchi yetu


        Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye

          Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) Shaban Matwebe

Na. Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amekutana na wanahabari kutoka Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) ambapo amewaasa kutumia vizuri majukwaa yao ya habari mtandaoni kujipatia kipato kukuza maisha yao. 

Waziri Nape ameyasema hayo alipokutana na wadau wa jumuiya hiyo tarehe 5 Julai, 2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam ili kujadili mambo mbalimbali ambayo yanahusu kuboresha tasnia ya habari mtandaoni.

“Tunafuatiliwa na watu wengi mtandaoni na wengi wanatuamini, wanatuelewa ninachotaka kuwaomba ni kwamba ni vizuri tutumie mitandao hiyo vizuri kwa sababu tuna nchi ambayo tuna wajibu wa kuilinda na kuendelea kuwa katika utulivu wajibu huo ni wetu sote”, alisema Waziri Nape.

Aidha, aliitaka jumuiya hiyo kama wanahabari kutimiza wajibu wa kufichua maovu huku ikitimiza wajibu wa kuilinda nchi, pia aliwataka wanahabari  kujikita katika utaalam wa  maeneo mbalimbali ili kuweza kuandika habari katika maeneo hayo.




No comments